Home ENTERTAINMENTS MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAMEKAMILIKA, WANANCHI WAOMBWA KUFURIKA

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAMEKAMILIKA, WANANCHI WAOMBWA KUFURIKA

Mkurugenzi wa Msama Promotion ambaye pia ni Mwandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama akionesha maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kesho siku ya Pasaka April 9,2023 katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo April 8, 2023 katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam litakalofanyika Katika Viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

Sehemu ya maandalizi ya tamasha hilo viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM.

Maandalizi ya tamasha kubwa la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kesho April 9, 2023 katika Viwanja vya Leader’s Club vilivyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam yamekamilika na kila kitu kipo sawa.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Msama Promotion ambaye pia ni Muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Leaders Club litakapofanyika tamasha hilo.

Msama amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika nakwamba, waimbaji wote wapo tayari kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kutoa burudani safi katika tamasha hilo.

Aidha ameongeza kuwa kutakuwa na maombi maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili na kufanya kazi kubwa ya kuiongoza nchi ya Tanzania.

“Mgeni rasmi kwenye tamasha letu ni RAIS wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye atawakilishwa na Waziri wetu wa Habari Nnape Nnauye, hii ni kutokana na majukumu makubwa aliyonayo Rais wetu ya kuliongoza Taifa letu,

“kutakuwa na maombi maalum ya kumshukuru Mungu kwa miaka miwili ambayo Raisi wetu ametuongoza vyema,

“Pia kutakuwa na michezo ya watoto, kubembea, kuselereka na mengine mengi. Naendelea kusisitiza kuwa hakuna kiingilio, tamasha hili litakuwa bure na usalama wa hali ya juu kwa watu na mali zao,  hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kufurika kwenye tamasha hili ili wajionee burudani itakayoacha gumzo” amesema Msama.

Waimbaji wa nyimbo za Injiri watakaoshiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na Masi Masilia kutoka Congo, Faustina Munishi kutoka Kenya, Tumaini Akilimali kutoka Kenya, Joshua Ngoma kutoka Rwanda, Nicole Ngabo kutoka Congo, Upendo Nkone, Abwene Mwasongwe na wengine wengi kutoka Tanzania.

Previous articleWAZIRI GWAJIMA APONGEZA KUONGEZEKA FURSA ZA UKOPESHAJI WANAWAKE
Next articleWAZIRI MKUU ATOA POLE MSIBA WA BRIG. GEN. MSTAAFU ALOYCE MWANJILE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here