Home ENTERTAINMENTS GETHSEMANE GROUP KINONDONI(GGK) WAACHIA VIDEO YA BWANA WASTAHILI

GETHSEMANE GROUP KINONDONI(GGK) WAACHIA VIDEO YA BWANA WASTAHILI

Na: Mwandishi Wetu

WAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa Bwana Wastahili.

Video ya wimbo huo imeachiwa leo Machi 18,2024 saa mbili usiku na imerekodiwa katika Studio ya Flying Wave Studio na kuongozwa na Director maarufu ajulikanae kama Director Joowzey.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya video hiyo kuachiwa hewani(kuzinduliwa) Mwenyekiti wa Gethsemane Group Kinondoni GGK Geoffrey Joseph amesema ni furaha kwao kuja na video ya wimbo huo ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumtukuza Mungu.

“Ujumbe mkubwa kwenye wimbo huu ni kwamba Mungu pekee ndie anastahili kuabudiwa na yeye ndiye anatosha kwa kila kitu hasa kipindi hiki ambacho baadhi ya madhehebu wapo Kwenye mfungo, tunaamini wimbo huu ni ibada na utawasogeza karibu zaidi na Mungu” amesema Joseph

Aidha ametoa neno kwa wasikilizaji na watazamaji wa video ya wimbo huo kutambua hakuna yoyote anayestahili kuabudiwa zaidi ya Mungu pekee.Previous articleDKT. NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA 11 WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA ( FLMS)
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 19-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here