Home LOCAL BALILE MWENYEKITI MPYA JUMUIYA YA WAHARIRI AFRIKA MASHIRIKI

BALILE MWENYEKITI MPYA JUMUIYA YA WAHARIRI AFRIKA MASHIRIKI

Jumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kuwa mwenyekiti wa jumuiya kwa kipindi cha Mwaka 2024 – 2025.

Pia imemchagua Fitihawok Yewondwossn, kutoka Jukwaa la Wahariri Ethiopia kuwa Makamu wa Rais kwa kipindi hicho.

Balile amechaguliwa baada ya kufanyika Mkutano Mkuu wa jumuiya hiyo nchini Ghana, ikiwa ni baada ya kumalizika kwa Kongamano la Tatu la Vyombo vya Habari Afrika lililofanyika Accra, Ghana wiki hii.

Akizungumza kwenye mkutano huo baada ya kuchaguliwa kuwa rais, Balile alisisitiza muhimu wa kupata taarifa kama haki ya msingi inayowezesha kupatikana kwa haki nyingine.

Alielezea umuhimu wa EAES kuhakikisha haki hiyo inapatikana na kufurahiwa na raia wote wa Afrika Mashariki na kwingineko.

Balile alisisitiza haja ya ushirikiano kati ya vyombo vya hanari na serikali, vyama vya siasa, jumuiya za kiraia, na jumuiya za kimataifa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama wake kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, na Ethiopia.

Previous articleMAJALIWA: WATANZANIA TUJIWEKEE UTARATIBU WA KUFANYA MAZOEZI
Next articleKIWANDA CHA KWANZA CHA KIZALISHA SARUJI NYEUPE CHAZINDULIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here