Home BUSINESS KIWANDA CHA KWANZA CHA KIZALISHA SARUJI NYEUPE CHAZINDULIWA

KIWANDA CHA KWANZA CHA KIZALISHA SARUJI NYEUPE CHAZINDULIWA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe (Mb) imezindua kiwanda Cha kwanza kwa ukanda wa nchi za Kusini Mwa Jangwa la Sahara,kinachozalisha saruji nyeupe kwa ajili ya ujenzi. Kiwanda hicho kilichoko eneo la wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani kina uwezo wa kuzalisha tani 200 Kwa siku,huku kikiongeza ajira na Mapato kwa nchi. Akizindua kiwanda hicho leo 18 Mei 2024.Mhe Kigahe amesema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hususani kupitia sekta ya viwanda Ili viweze kuchangia katika kuongeza fursa mbalimbali, kupitia kiwanda hicho kitaongeza fursa za ajira, kuongeza fedha za kigeni na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Aidha Kigahe amesema serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara itashirikiana na kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho zinavuka mipaka ya nchi na kufika hata katika soko huru la Afrika. Aidha amezitaka halmashauri mbalimbali kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali pamoja na kutenga maeneo ya uwekezaji Kwa kuwa serikali imeweka mazingira yanayovugia uwekezaji. “Kuwekeza nchini Tanzania ni sehemu salama na yenye mazingira yaliyoboreshwa ambayo kila mwekezani ataweza kunufaika na wananchi nao kunufaika, na kuongeza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya kupunguzwa umaskini na kukuza uchumi wa nchi” .Amesema Kigahe Amesema kiwanda hicho mbali ya kuongeza thamani ya uzalishaji lakini pia ni sehemu ya kuitangaza Tanzania kutokana na uzalishaji huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Bw. Prem Ahuja Amesema kuwa Kiwanda hicho cha saruji nyeupe kinasimama kama ushuhuda wa dhamira ya Ubunifu wa Ubora na Uendelevu, ni ahadi ya kuwa hii ni fursa kubwa kutokana na kwamba saruji inayozalishwa hapa kazi yake kubwani kuboresha sekta ya ujenzi” Amesema Ahuja.
Nae mkuu wa wilaya ya Mkuranga,Hadija Nasri amesema uwekezaji huo ni heshima na imetokana na kuwepo Kwa mazingira mazuri ya uwekezaji, Wilaya ya Mkuranga ina viwanda 123 na inajivunia kwa kuwa na mazingira wezwshi Tanzania.
Previous articleBALILE MWENYEKITI MPYA JUMUIYA YA WAHARIRI AFRIKA MASHIRIKI
Next articleWAZIRI MKUU ATOA TUZO ZA MALKIA WA NGUVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here