Home Uncategorized SHULE YA SEKONDARI MCHANGANYIKO WAJIVUNIA MAFANIKO KITAALUMA

SHULE YA SEKONDARI MCHANGANYIKO WAJIVUNIA MAFANIKO KITAALUMA

Mkuu wa shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko ABEID KAMUGISHA akimpa hotuba mgeni rasmi Fatuma Abubakari Mwakirishi wa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam OMARY KUMBILAMOTO Katika mahafali ya kidato Cha nne Leo Octoba 20/2022 ambapo jumla ya Wanafunzi 392 wamehitimu elimu ya Sekondari Katika mahafali ya 12 (Picha na Heri Shaaban)

Diwani wa Kata ya Gerezani Fatuma Abubakari akivushwa Skafu na Skauti wa WIlaya ya Ilala Leo shule ya sekondari Uhuru Mchanganyiko wakati wa Mahafali ya Kidato Cha nne ,Diwani Abubakari amemwakilisha Meya wa Halmashauri ya Jiji OMARY KUMBILAMOTO Katika mahafali hayo ambayo Jumla ya Wanafunzi 392 Leo wamehitimu elimu ya Sekondari (NA HERI SHAABAN).

Wanafunzi wa Kidato Cha Nne shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko wakiwa katika mahafali ya Kumi na mbili Leo Octoba 20/2022 ambapo jumla ya Wanafunzi 392 wamehitimu Elimu ya Sekondari (NA HERI SHAABAN)

Na: Heri Shaaban (Ilala)

SHULE ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko wajivunia Mafanikio kitaaluma katika MATOKEO ya kidato cha pili na kidato cha nne kila mwaka wanafaulisha kwa kiwango cha juu.

Akizungumza katika mahafali ya 12 ya kidato cha nne Shuleni hapo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Uhuru Mchanganyiko ABEID KAMUGISHA alisema shule hiyo ilianza mwaka 2007 ikiiwa na walimu nane na Wanafunzi 160 kwa Sasa mwaka 2022 shule ina Walimu 38 kati yao wanaume 14na WANAWAKE 24 na wafanyakazi wanne .

“Kitaaluma shule inafanya vizuri kila Mwaka Mwaka Jana matokeo ya kidato cha nne yaliotangazwa na NECTA ilifanikiwa kufaulisha kwa asilimia 77 na matokeo ya mtihani wa mock tumefaulisha kwa asilimia 80 Mwaka huu 2022 watoto wetu watafaulu kwa kiwango Cha juu tumewandaa kwa Mazingira mazuri ” alisema Kamugisha.

Aidha alisema pia Wanafunzi wa Kidato cha pili wa shule hiyo Uhuru Mchanganyiko ambao wanatarajia kufanya mtihani wa NECTA Novemba 2022 takwimu za NECTA 2021 ufaulu ulikuwa asilimia 91 hivyo Vijana wetu wa Mwaka huu watafanya vizuri zaidi .

Mkuu wa shule aliwataka Wanafunzi wanaomaliza kujiendeleza Kielimu mpaka chuo kikuu aliwataka wajilinde wasijitumbukize Katika vitendo viovu Vya utumiaji wa madawa ya kulevya

“Nawaomba vijana wetu msome kwa bidii mzingatie masomo yenu Elimu aina mwisho nawaomba mzingatie masomo muweze kufika chuo kikuu “ alisema Kamugisha

Kwa upande wa risala ya wahitimu wa kidato Cha nne iliyosomwa na Zuhura Maulid alisema shule ya Sekondari uhuru Mchanganyiko ina mchepuo wa Sayansi ,Sanaa na Biashara

Zuhura alisema jumla ya wahitimu mwaka huu 2022 392 kati ya yao wavulana 196 na Wasichana 196

Zuhuru alitoa ushauri Kwa Serikali wanaomba kuongezewa Walimu wa Sayansi na chumba cha kompyuta kwa ajili ya Wanafunzi kusoma Somo la TEHAMA .

Aidha alitoa wosia kwa Wanafunzi wanaobaki wawe na maadili mema wawatii Walimu wawe na nidhamu wasome kwa bidii waweze kufikia malemgo yao.

Mgeni rasmi Diwani Fatuma Abubakari aliyemwakilisha Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto aliwaasa Wahitimu wa shule hiyo kuzingatia nidhamu wawapo shuleni Ili waweze kusonga mbele mpaka chuo kikuu .

Mwakilishi wa Meya Diwani Fatuma Abubakari alisema atafatilia Halmashauri mikakati ya ujenzi wa Shule ya gholofa Ili uweze kuanza mara moja .

Alisema pia atatatua changamoto za shule hiyo zikiwemo upungufu wa Walimu wa masomo ya sayansi 

Previous articleRAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA  DKT. MWINYI MAKAME HAJI
Next articleKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO YAKUTANA DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here