Home LOCAL RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA  DKT. MWINYI...

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA  DKT. MWINYI MAKAME HAJI

 
 
TAARIFA KWA UMMA
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Dkt. Mwinyi Haji Makame aliyewahi kuwa Muwakilishi wa Jimbo la Dimani na Waziri katika Wizara mbalimbali,  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilichotoke usiku wa kuamkia tarehe 20 Oktoba, 2022 nyumbani kwake Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amemuelezea Marehemu Dkt. Mwinyi Haji Makame ni kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika uhai wake, kuleta maendeleo kwa wananchi na serikali kwa ujumla katika utumishi wake akiwa katika nyadhifa mbali mbali.

“Tumepoteza Kiongozi na Mwanachama muaminifu wa CCM aliyeitumikia nchi yetu kwa uadilifu, umakini na uhodari mkubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo ndani ya Chama na Serikali kwa vipindi vyote ambavyo alitumikia akiwa katika nyadhifa mbali mbali za utumishi wake” Ndugu Samia Suluhu Hassan

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa pole kwa familia ya Marehemu, Ndugu, Jamaa, Marafiki.

Marehemu Dkt. Mwinyi Haji Makame amekuwa Muwakilishi wa Jimbo la Dimani tokea mwaka 2000 hadi 2020 ambapo aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali na Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuwahi kuwa  Waziri wa Fedha na Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Ameni.

Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Tutarejea.


Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Itikadi na Uenezi
21 Oktoba, 2022

Previous articleJOPO LA MAAFISA KUTOKA PEPFAR, CDC, PeaceCorps, DOD & USAID LAKUTANA NA MABINTI BALEHE NA AKINA MAMA VIJANA KAHAMA
Next articleSHULE YA SEKONDARI MCHANGANYIKO WAJIVUNIA MAFANIKO KITAALUMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here