Home LOCAL WAHAMIAJI HARAMU 77 RAIA WA BURUNDI WAKAMATWA GEITA.

WAHAMIAJI HARAMU 77 RAIA WA BURUNDI WAKAMATWA GEITA.



Na, Costantine James  Geita.

Wahamiaji haramu 77 Raia wa Burundi wamekamatwa mkoani Geita kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria huku wakijihusisha na shughuli za kuendesha Baisikeli mkoani  humo.

 Wahamiaji hao wamekamatwa katika maeneo mbali mbali mkoani Geita kufuatia oparesheni inayoendeshwa mkoani Geita na idara ya uhamiaji kwa lengo la kuwabaini raia wa kigeni walioingia nchini kinyume na sheria.

Afisa uhamiaji Mkoa wa Geita kamishina msaidizi wa uhamiaji Emmanuel Lukumai amesema mpaka sasa wamekamata raia  wa Burubdi 77  wanao endesha baisikeli huku wengine wakifanya shughuli mbalimbali za mashambani ambao wameingia nchini kinyume na sheria.

Kamishina Emmanuel amesema Raia hao wameingia nchini kinyume na sheria  za nchi kwa lengo la kujishughulisha na shughuli mbali mbali ikiwemo kuendesha baiskeli nakufanya shughuli za mashambani.

Amesema wahamiaji hao baadhi yao watafikishwa mahakamani huku wengine watatozwa faini maarumu kamishina Emmanuel amewataka  wakazi wa  mkoa wa Geita kuacha tabia ya kuishi na Raia wa kigeni kinyume na sheria.

“Wito wangu kwamba wasipende kukaa na raia wa kigeni ambao hawajafata taratibu kama anamhitaji  mtu afate taratibu zote za kiuhamiaji anapokuwa nchini” Amesema  Afisa uhamiaji Mkoa wa Geita kamishina msaidizi wa uhamiaji Emmanuel Lukumai.

Wizey  Yohani, Ninyonzima Khalfani na Nyawenda Rajabu, Ni miongoni mwa Raia 77 wa Burundi waliokamatwa mkoani Geita wamekili kuingia nchini Tanzania kinyume na taratibu za uhamiaji   wamesema  sababu za kuzamia nchini Tanzania ni maisha magumu waliyo nayo.
Previous articleNAIBU WAZIRI GEKUL AWATAKA WASANII KUWA MABALOZI WAZURI WA WIMBO WA TAIFA
Next articleMTOTO WA MIAKA 7 AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI GEITA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here