Home ENTERTAINMENTS NAIBU WAZIRI GEKUL AWATAKA WASANII KUWA MABALOZI WAZURI WA WIMBO WA TAIFA

NAIBU WAZIRI GEKUL AWATAKA WASANII KUWA MABALOZI WAZURI WA WIMBO WA TAIFA

Naibu waziri wa utamaduni ,sanaa na michezo Pauline Gekul akizungumza na wasanii wa chama cha uigizaji Tanzania (TDFAA) katika mkutano wao uliofanyika jijini Arusha.
Baadhi ya wasanii walioshiriki mkutano wa chama cha waigizaji Tanzania (TDFAA) jijini Arusha

Mwenyekiti wa chama cha waigizaji Tanzania (TDFAA) Slum Mchoma, akizungumza kwa niaba ya wasanii wa chama hicho katika mkutano wao uliofanyika jijini Arusha.

Na: mwandishi wetu,Arusha.

Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo,Pauline Gekul  amewataka wasanii nchini kuwa mabalozi wazuri wa  wimbo wa Taifa, ili kuhakikisha hakuna mtu anayeweka vionjo vingine nje ya vilivyoasisiwa.

Gekul aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA) unaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha na kubainisha kuwa  kimsingi wimbo huo haupaswi kuchezewa kwa kuingiza vionjo au madogo mengine nje ya vilivyopo.

“Nawaomba nyie muwe mabalozi wa kulinda wimbo wetu huu ambao umeasisiwa na unaonyesha utaofa wetu,haifai kuongizwa madoido mengine  ambayo hayaleti utaifa wetu kama ulivyoasisiwa na wasisi wetu, unapaswa kubaki na usajili wake,”alisema

Gekul alisema,fani ya uigizaji inamchango mkubwa kwa Taifa, kwani wamekuwa washiriki wazuri hasa wa kusimama mstari wa mbele kwenye kuhamasisha masuala mbalimbali ya Taifa.

“Kama wakati ule wa vita ya Nduli Idd Amini wasanii walishiriki kutunga nyimbo mbalimbali za kuhamasisha kumpigia adui huyo ili Taifa letu kibali salama,lakini katika vita dhidi ya Uviko-19 na Ukimwi pia tumeona,”alisema naibu waziri huyo.

Aidha,alisema kutokana na umuhimu huo Rais Samia Suluhu kaona umuhimu wa kufufua Mfuko wa  Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa kwa kuwapatia zaidi ya Sh.bilioni 1.4 ili kuwania kiuchumi waigizaji nchini.

Alisema kupitia fedha hizo wanaweza kukopa kwa riba nafuu na kuendeleza kazi zao huku wakichangia kukuza uchumi wa Taifa na wao binafsi.

Kuhusu ombi lao la kumuomba Rais Samia awe mgeni rasmi katika kongamano lao,alisema viongozi waandae ratiba rasmi na kufikisha wizarani ili ampigie Rais na anaamini anasikiliza ombi hilo huku akiwataka hao  waigizaji kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri nchini ili nao wanufaike nayo.

“Suala lenu mlilonipa hapa la  kupunguza kodi alisema Bodi ya Filamu ilikutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kupunguza kodi na tozo za wasanii na linafanyiwa kazi,”alisema

Aliwaasa kudumisha  umoja na upendo walionao ili chama chao kistawi na kufanya mambo makubwa zaidi ya kuinua Tania hiyo.

Gekul aliwaomba pia kuhakikisha wanapeleka chama hicho katika kila mkoa ambapo kwa sasa wapo  mikoa 22 kati ya 26 licha ya mikoa yote kuwa na wasanii.

Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA) Salum Mchoma alisema chama hicho kinawachama hai 36,714  na kusisitiza kuwa wanamahitaji mbalimbali, kwani uigizaji ni rasilimali na kazi yao kubwa   kuikumbusha serikali na jamii kuwa sanaa ni muhimu katika uchumi wa nchi.

Alisema Tanzania inazaidi ya wasanii milioni 6 kati yao wasanii milioni 3 wanatokana na kazi za uagizaji lakini hawapo pamoja, hivyo vema serikali  kuwakusanya pamoja ili  kuwasaidia kutambulika.

Alisema sekta hiyo inamuingiliano wa aina mbalimbali na sekta mbalimbali hivyo alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kuwakumbuka na kuwakwamua kiuchumi kwa kuwapa Sh,bilioni 1.5 katika  mfuko wao, utakaowezesha kukopa kwaajili ya kujikwamua kiuchumi.

Pia waliomba kutambuliwa na Wizara ya Utumishi na Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)kwani zinashikilia fedha kwaajili ya vijana,ajira na watu wenye ulemavu na kuomba chama hicho kitambuliwe ili wapate fedha za mikopo  ili waigizaji wapate maendelo na kujikwamua kiuchumi

“Tunaomba maafisa utamaduni watupokee vivyo hivyo ili tusikwame kimaendeleo pia tunaomba kupunguziwa na kuondolewa kodi na tozo ya kazi kwa wasanii ili  tusiwe na mzigo mkubwa wa gharama za kazi zetu,”alisema.

Alisema wanaishukuru Taasisi ya Haki Miliki Tanzania ( Cosota) kwakuwasaidia wasanii  pale wanapohitaji msaada wao.

Naye Msemaji wa Yanga na balozi wa kampuni ya GSM,Haji Manara alitoa rai kwa wasanii nchini kutumia  misingi ya Azimio la Arusha kwaajili ya kujikwamua kiuchumi kwani hali iliyopo hivi sasa kwa wasanii si ya kuridhisha kutokana na baadhi yao kuwa na majina makubwa lakini uhalisia wa kimaisha duni.

Previous articleMGONGOLWA: RAIS SAMIA AMEONESHA THAMANI HIFADHI ZA JAMII, VIONGOZI WAELEZENI WANANCHI
Next articleWAHAMIAJI HARAMU 77 RAIA WA BURUNDI WAKAMATWA GEITA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here