Home LOCAL MTOTO WA MIAKA 7 AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI GEITA.

MTOTO WA MIAKA 7 AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI GEITA.


Na. Costantine James,  Geita.

Mtoto wa maiaka  7  John Frank  Mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi nguzo mbili  Mkoani Geita  amefariki dunia wakati akipelekwa hosibitalini kupatiwa matibabu  baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara  kuelekea shuleni.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Geita kamishina msaidizi Henry  Mwaibambe emedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo  amesema  chanzo cha ajali  ni uzembe wa dereva wa gari iliyosababisha ajali hiyo.

Mwaibambe amesema mpaka sasa wanamshikilia dereva wa  gali lililo sababisha ajali lenye usajili namba T 177 AHH,  aina ya  Isuzu Tipa dereva huyo ametambulika kwa jina la Renatus Christopher  mwenye umri wa miaka 31  wanamshikilia kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Mwaibambe amesema eneo hilo  linawatu wengi kutokana na kuwepo shule mbili katika eneo hilo, Shule ya Msingi Nguzo mbili, Shule ya msingi Mwatule  amesema kufuatia ajali hiyo jeshi la polisi wamechukua hatua ya kuweka asikali wa usalama barabarani ili kuwavusha watoto katika eneo hilo.

“Imetokea ajali  leo majira ya saa tano asubuhi eneo la mwatulole  ambapo mtoto wa darasa la kwanza aitwaje John Frank mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Nguzo Mbili  amefaliki dunia wakati akipelekwa hosipitali kupatiwa matibabu hospitalini” Amesema Kamanda Mwaibambe.

Baadhi ya  wananchi wa Mwatulole ambao ni mashuhuda wa ajali hiyo wamesema  eneo hilo limekuwa hatalishi kutokana na kuwepo kwa wanafunzi wengi.

 Wananchi  pamoja na wazazi wameiomba serikali  kuweka alama za barabarani  katika eneo hilo ili kupunguza  ajali  kwa wanafunzi  wanaosoma  katika shule ya msingi Nguzo mbili na mwatulole  kwani madereva wa malori wamekuwa  wakipita kwa kasi katika eneo hilo.
Previous articleWAHAMIAJI HARAMU 77 RAIA WA BURUNDI WAKAMATWA GEITA.
Next articleWAZIRI NDALICHAKO ATAKA MUONGOZO WA SADC WA KULINDA AJIRA KWA WATOTO KUZINGATIA MAADILI YA KIAFRIKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here