Home BUSINESS SERIKALI KUPITIA MKUMBI YAFUTA TOZO NA KERO 231

SERIKALI KUPITIA MKUMBI YAFUTA TOZO NA KERO 231

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara Jijini Dar es Salaam, Dkt. Yonazi pia ni Mwenyekiti wa Kikosi kazi hicho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga na Kushoto ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikundi Kazi hicho cha Mazingira ya Biashara, Bw. Vicent Minja

Na. Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) imefuta na kupunguza jumla ya tozo, ada na faini zisizopungua 232 kati ya 380 zilizobainishwa katika utekelezaji wake sawa na asilimia 61.

Akizungumza wakati wa Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifungua Tanzania na kuwa kivutio cha kufanya biashara na uwekezaji inatekelezeka kwa vitendo kwa ufutwaji wa tozo, ada na faini ambazo zilikuwa kero kubwa kwa ustawi, ukuaji na maendeleo ya biashara na uwekezaji hapa nchini.

Previous articleRAIS MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI ZANZIBAR
Next articleRAIS WA ROMANIA AWASILI RASMI NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here