Home LOCAL RAIS WA ROMANIA AWASILI RASMI NCHINI

RAIS WA ROMANIA AWASILI RASMI NCHINI

Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis, amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa kuanzia leo tarehe 16 hadi 19 Novemba 2023 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)

Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kushawishi uwekezaji zaidi na kuvutia watalii wengi kutoka nchini Romania.

Aidha katika mazungumzo rasmi yatakayofanyika tarehe 17 Novemba 2023 Rais huyo na mwenyeji wake watajadili namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati sekta za elimu, afya, kilimo nishati na madini.

Kabla ya kuondoka nchini tarehe 19 Novemba 2023 Rais wa Romania atapata fursa ya kwenda Zanzibar ambapo atazungumza na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kutembelea mji mkongwe ambao ni moja kati ya vivutio vikubwa vya utalii duniani.

Previous articleSERIKALI KUPITIA MKUMBI YAFUTA TOZO NA KERO 231
Next articleSERIKALI YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WAKE KATIKA KIWANDA CHA SUKARI CHA TPC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here