Home LOCAL RAIS MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI ZANZIBAR

RAIS MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI ZANZIBAR

Na: Halfan Abdulkadir – Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko madogo kwa kuwateuwa viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Mikoa visiwani humo.

Taarifa ya Ikulu ilivyotolewa leo November 16, 2023 imesema Rais Mwinyi amemteua Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amemteua Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Pia amemteua Sadifa Juma Khamis kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.

Amemteua, Othman Ali Maulid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja. Kabla ya uteuzi huo, Maulid alikuwa Mstaafu wa Utumishi wa Umma.

Amemteua, Galos Nyimbo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja. Nyimbo ni Mwanajeshi Mstaafu.

Taarifa hiyo imesema kuwa wateule wote wataapishwa Septemba 20, 2023 saa 3:00 Asubuhi Ikulu, Zanzibar.

Previous articleMWANAMITINDO JASINTA MAKWEBE KUIWAKILISHA TANZANIA MASHINDANO YA FUTURE FACE 2023 NIGERIA
Next articleSERIKALI KUPITIA MKUMBI YAFUTA TOZO NA KERO 231
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here