Home BUSINESS WANANCHI WAPATA MWITIKIO MKUBWA USAJILI WA MILIKI UBUNIFU BRELA

WANANCHI WAPATA MWITIKIO MKUBWA USAJILI WA MILIKI UBUNIFU BRELA

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Wananchi mbalimbali wamejitokeza katika Banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kupata huduma mbalimbali zinazotolewa wa Wakala huyo ikiwemo kusajili Bunifu zao katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano. BRELA, Bi. Rhoida Andusamile amesema, wananchi wamepata muitikio mkubwa kutembelea Banda lao  katika maonesho hayo.

Amesema kuwa BRELA imekuwa na utaratibu wa kushiriki kila mwaka maonesho hayo na kutoa huduma za hapo kwa papo jambo linalopelekea watu wengi kuhamasika.

“Mwaka huu tumekuja kivingine, tuna mabanda manne ambayo tunatoa huduma za umiliki ubunifu, Banda lingine huduma zote kwa ujumla, na mabanda mawili ni kwa ajili ya huduma za papo kwa papo ambapo tumeona tutumie fursa hii kuwa na Banda la umiliki ubunifu, ni kutokana na wananchi wengi kuwa na uelewa mdogo katika maswala ya miliki bunifu, hivyo basi tumeona tutumie fursa hii kuwahamasisha wabunifu na wavumbuzi mbalimbali kusajiri vumbuzi zao ili waweze kunufaika nazo” amesema Bi. Rhoida.

Amewasihi wambumbuzi mbalimbali kutumia fursa hiyo ili kulinda kazi zao na kukabiliana na changamoto ya kuibiwa kazi zao, kwani kuna wavumbuzi wengi wameingia kwenye changamoto hiyo  kwa kushindwa kuzilinda kwa kuzisajili.

“Kwa hiyo tunawahamashisha hasa wasomi kwenye vyuo vya ufundi wafike au wapate huduma za BRELA hii siyo Taasisi ya Biashara, ni Taasisi ya Huduma, hivyo wafike hapa au wawasiliane na wataalamu wetu ili wapate utaratibu wa kusajiri vumbuzi zao,”alisema.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 4,2023
Next articleTTCL YAJIVUNIA UKUAJI WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KWA KUTANGAZA UTALII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here