Home BUSINESS TANZANIA COMMERCIAL BANK, LIFE INSURANCE WAZINDUA ‘ADABIMA’ KUMSAIDIA MWANANCHI KULIPA ADA ZA...

TANZANIA COMMERCIAL BANK, LIFE INSURANCE WAZINDUA ‘ADABIMA’ KUMSAIDIA MWANANCHI KULIPA ADA ZA SHULE

DAR ES SALAAM

Tanzania Commercial Bank (TCB), kwa kushirikiana na kampuni ya Metro Life Assurance wamezindua BimaBenki yenye lengo la kutoa huduma mbili za Bima ziitwazo ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mei 17,2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware amesema kiini cha huduma hizo ni kutoa uelewa wa umuhimu wa elimu katika kujenga kesho bora ya jamii.

kuhusu ADABIMA, Dkt. Baghayo amesema huduma hiyo ni maalum kwa ajili ya ada ya shule inayokamilisha kiu ya mzazi au mlezi kumwona mtoto wake akifanikiwa kwa kupata elimu bora anayostahili ambapo bidhaa hiyo ilithibitishwa na Mamlaka mnamo tarehe 22 Novemba 2023.

“Kama tujuavyo wote, majanga ni jambo lisiloepukika katika maisha yetu. Si mara zote mipango yetu inatimia kama tunavyokusudia. Majanga hutokea katika nyakati tusizotegemea na kuvuruga mipango yetu na  familia zetu.

“ADABIMA ni suluhisho la changamoto hizi za maisha, lakini pia  ni ahadi kwa wateja kwamba lolote litakalotokea kampuni yake itasimama pamoja naye kuhakikisha mtoto anasoma  na kuhitimu masomo yake bila kadhia yoyote ile.” Amesema Dkt. Baghayo.

Kuhusu Saccoss Schemes Credit Life Insurance, Dkt. Baghayo amesema ni huduma ya Bima maalum kwa ajili ya wadau wa SACCOS na vikundi vya huduma ndogo za fedha (micro-finance).

Ameeleza kuwa Mamlaka itahakikisha huduma hiyo inaendelea kuwapa watumiaji usalama wa kifedha, utulivu, kujiamini na amani.

“Wadau hawa wanajenga kesho iliyo bora kwa kuinua uwezo wa watoa mikopo na kuwahakikishia wakopaji usalama na umiliki wa mali zao endapo watashindwa kulipa.” Ameeleza

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Bima kutoka Benki ya TCB, Francis Kaaya amesema Bima hizo ni kielelezo cha dhamira ya Benki ya TCB ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kadri ya mahitaji yao na kuwahudumia watanzania kwa ujumla.

“Tunaelewa umuhimu mkubwa wa elimu katika kujenga kesho bora ya jamii yetu. Bima hii inawapa usalama wa kifedha, lakini pia inalea ndoto na matarajio ya wateja wetu.

“Bima hizi ni kielelezo cha dhamira ya TCB Benki ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kadiri ya mahitaji yao na kuwahudumia Watanzania wote kwa ujumla.” amesema Kaaya.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya TCB, Jema Msuya amesema kama Taasisi za kifedha wanawajibu wa kumlinda mteja juu ya sintofahamu na majanga, lakini pia wateja wao wanafikia ndoto zao bila wasiwasi.

Nay,  Afisa Mkuu Idara ya fedha, Metro Life Assurance, Clifford Mkandala amesema kupitia ushirikiano wao na Benki ya TCB wanajivunia kuwaletea watanzania huduma ya Bima kadri ya mahitaji yao lakini pia kuvisaidia vikundi vya huduma ndogo za fedha.

“Tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na SACCOS pamoja na Vikundi vya huduma ndogo za fedha (micro-finance) katika kuimarisha uchumi na jamii yote nchini, kupitia ushirikiano wetu na TCB Benki, tunajivunia kuwaletea Watanzania huduma ya Bima kadiri ya mahitaji yao, na pia kuvisaidia Vikundi vya huduma ndogo za fedha.

“Ushirikiano kati ya TCB Benki na Metro Life Assuarance ni mfano wa dhamira ya pamoja ya kuleta ubunifu ili kumridhisha mteja” amesema Mkandala.

Previous articleMAJALIWA: MICHEZO NI NYENZO MUHIMU INAYODUMISHA AMANI
Next articleRAIS DKT. SAMIA ANAGUSWA NA MAISHA YA WATANZANIA-MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here