Home BUSINESS BoT YATUNUKIWA CHETI KWA KUANDAA MKATABA WA HUDUMA KWAMTEJA

BoT YATUNUKIWA CHETI KWA KUANDAA MKATABA WA HUDUMA KWAMTEJA

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetunukiwa cheti kwa kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja na kuwa mfano kwa taasisi ambazo bado hazijafanikiwa kukamilisha mkataba huo. Pia, cheti kimetolewa kwa Chuo cha BoT kilichopo jijini Mwanza ambacho pia kimeandaa Mkataba wake wa Huduma kwa Mteja kutokana na upekee wa shughuli zake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, alikabidhi vyeti hivyo kwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Yamungu Kayandabila, pamoja na kwa viongozi wa taasisi nyingine ambazo pia zimeandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja katika hafla iliyofanyika Nyerere Square jijini Dodoma.

Mkataba huo wa Huduma kwa Mteja unaelezea huduma ambazo BoT itatoa na muda wa utekelezaji wa huduma hizo kwa wananchi na wadau wake.

Waziri Simbachawene ameziagiza taasisi zote nchini kuandaa na kuhuisha Mikataba ya Huduma kwa Mteja na kuitumia katika utekelezaji wa majukumu yao ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza katika kilele cha wiki ya Utumishi wa Umma Simbachawene amezipongeza taasisi zote zilizokamilisha uandaaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja kwa kuwa mkataba huo utaongeza chachu katika utendaji wa kazi na kuleta ufanisi na tija katika taasisi na hivyo wananchi kupata huduma bora kama wanavyotarajia.

Aidha, amezitaka taasisi zote nchini kutumia mfumo wa e-mrejesho ambao unaonyesha mwanzo wa mwananchi kupata huduma na namna tatizo lake lilivyoshughulikiwa na kupata mrejesho kwa wakati.

Akizungumzia maadili katika utumishi wa umma Waziri Simbachawene amesisitiza kila mtumishi kuvaa kitambulisho chenye jina na cheo chake muda wote awapo katika maeneo ya kazi huku akisema kuwa uzalendo ni kutoa huduma bora kwa wananchi.

Previous articleDR. TAX AFANYA ZIARA CHUO CHA DIPLOMASIA INDONESIA
Next articleTANTRADE NA UBALOZI WA IRAN YAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here