Home BUSINESS TANTRADE NA UBALOZI WA IRAN YAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

TANTRADE NA UBALOZI WA IRAN YAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

23 Juni, 2023, Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi.Latifa M. Khamis amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Hussein Alvandi Behineh, Balozi wa Iran nchini yaliyofanyika katika Ofisi za Balozi tarehe 23 Juni, 2023.

Lengo la kikao hicho ni kujadili ukuzaji wa mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania na Iran Katika Biashara na Uwekezaji kwa Sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na afya, elimu na teknolojia.

Katika kikao hicho wamejadili kuhusu ushiriki wa Iran kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo kutakuwa na siku maalum ya Iran kwa ajili ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Iran ili kubadilishana fursa baina yao.
Sambamba na hilo walijadili kuhusu kuratibu misafara ya kisekta zikiwemo afya, elimu na teknolojia mbalimbali.

Previous articleBoT YATUNUKIWA CHETI KWA KUANDAA MKATABA WA HUDUMA KWAMTEJA
Next articleCOSTECH: KUENDELEZA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KWA MAENDELEO YA TAIFA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here