Home BUSINESS CHAMA CHA WASTAAFU WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOTRA) WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI,...

CHAMA CHA WASTAAFU WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOTRA) WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI, KUPITISHA MPANGO KAZI 2023.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe akifungua mkutanomkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam Aprili 27,2023.

NA:  JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.

Wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi nchini wametakiwa kuwa na utamaduni wa kujiandaa mapema kustaafu kwa kutengeneza mazingira rafiki ya kiuchumi jambo ambalo litawasaidia kuishi maisha ya heshimu katika jamii kipindi wanapostaafu.

Akizungumza lo tarehe 27/4/2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Mwaka, Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe, amesema mkutano mkuu huo umelenga kufanya uchaguzi wa viongozi, kujadili mpango mkakati, Bajeti pamoja na kupitisha mpango kazi wa mwaka 2023.

“Tunatarajia katika mkutano huu kuchangua viongozi watakaotuongoza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo” amesema Bi. Rubambe.

Bi. Rubambe amesema kuwa lengo la Chama hicho ni kujitoa katika kusaidia na kufanya kazi za jamii pamoja na kuendeleza umoja na mshikamano na mahusiano kwa wastaafu hao ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwa wastaafu kwa vijana ambao wako kazini na wanaoingia kazini kwakuwa ni wastaafu watarajiwa.

“Wakati umefika kwa wafanyakazi kujipanga na kujiandaa mapema kustaafu ili kuleta tija katika maisha” amesema Bi. Rubambe.

Miongoni mwa washiriki katika mkutano mkuu wa mwaka alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba ambapo ameshiriki kama mwanachama wa heshima.

Naibu Gavana mastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Bernald Kibese  ambaye  pia ni Mwanachama wa heshima  ameshukuru chama cha BOTRA kwa kuwaalika wanachama wa heshima wa BOTRA katika mkutano mkuu huo ambapo pia amewatakia mkutano mwema ili malengo ya mkutano yakatimie.

Naye  Afisa Usajili Kanda ya Mashariki Bi. Salama Semakalila ambaye amemuwakilisha Bw. Emmanuel Kihampa Msajili wa Jumuiya za Kiraia amewataka wastaafu hao kuhakikisha wanafanya uchaguzi na kupata viongozi ikiwa ni pamoja na  kuepusha migogoro isiyoya ya lazima pamoja na kuhakikisha wanapeleka katika ofisi ya msajili taarifa zote za mkutano huo mkuu ili uweze kupata baraka msajili. 

Naibu Gavana mastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Bernald Kibese  akitoa salamu zake kwa niaba ya wanachama wa heshima wa chama cha wafanyakazi wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania BOTRA kwenye mkutano uliofayika kwenye ukumbi wa BoT jijini Dr Esa Salaam.

Afisa Usajili wa Jumuiya za Kiraia  Kanda ya Mashariki Bi. Salama Semakalila akizungumza katika Mkutano Mkutano Mkuu wa BOTRA uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe pamoja na viongozi wengine wakisimama kwa ajili ya kuwakumbuka wananchama wastaafu waliotangulia mbele ya haki.

Picha mbalimbali zikionesha wastaafu wakishiriki katika mkutano mkuu huo wa mwaka.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO APRILI 28, 2023
Next articleNAIBU KATAMBI AELEZA HATUA ZA UANZISHWAJI MFUKO WA TAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea CHAMA CHA WASTAAFU WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOTRA) WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI, KUPITISHA MPANGO KAZI 2023.