Home LOCAL TGNP YAFANYA TATHMINI YA MATOKEO YA KUKUA KWA TAPO LA UFEMINIA...

TGNP YAFANYA TATHMINI YA MATOKEO YA KUKUA KWA TAPO LA UFEMINIA NGAZI YA JAMII

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi 

Na Deogratius Temba

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umewakutanisha washiriki 30,
wawakilishi wa mashirika na vikundi kutoka mikoa tisa ya mradi wa Ujenzi wa
TAPO la Ukombozi wa wanawake  na
uimarishaji wa harakati za kupigania Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia
nchini Tanzania.

Mradi huu unaojulikana kama 
“Sauti za Wanawake na Uongozi”
unaofadhiliwa na Ubalozi wa Canada (GAC)
unalenga kuhakikisha kila mwanajamii anatambua umuhimu wa haki za wanawake,
usawa wa Kijinsia na kusimamia misingi ya Haki na Usawa wa Kijinsia katika
utendaji wa kila siku katika jamii. 

Warsha ya siku mbili (2)
inayofanyika katika Ofisi za TGNP, imejikita katika kuvuna matokeo ya
mafunzo ya ufeminia waliyopatiwa hapo awali kwa lengo la kutambua michango ya
mashirika mbalimbali na vikundi katika kuendeleza na kuimarisha vuguvugu la
utetezi wa haki za wanawake.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwamba mradi huo unalenga kuhakikisha
vuguvugu la harakati za kutetea Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia
linasambaa,  ili jamii yote izingatie
msingi ya usawa wa kijinsia. 

“Tunatamani kuona kila mtu katika taifa letu akiwa na uelewa
wa masuala ya usawa wa kijinsia na kuhsehimu haki za binadamu. Nyie ambao
mnatokea kwenye taasisi na vikundi mbalimbali katika ngazi ya jamii, ndio
mmepewa jukumu la kusambaza hii elimu na kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu
usawa wa Kijinsia na Haki za wanawake. Tunategemea kuona mabadiliko makubwa
sana huko mlinakotokea” alisema Liundi

Previous articleWASANII KUUNGWA MKONO KUENDELEZA TAALUMA YAO: DKT. MPANGO
Next articleTANZANIA YAVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UZALISHAJI WA CHAKULA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here