Home BUSINESS TANZANIA YAVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UZALISHAJI WA CHAKULA 

TANZANIA YAVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UZALISHAJI WA CHAKULA 

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Miungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji ikiwemo sekta ya uzalishaji wa chakula ili kuvutia wawekezaji katika sekta

kuzalisha kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya ndani na nje nchi.

Ameyasema hayo Novemba 8, 2022 alipokuwa akishiriki katika Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Chakula na Teknolojia zinavyowezesha uzalishaji wa chakula kwa kuzingatia viwango na mahitaji ya kimataifa bila kuathiri afya na mazingira unaofanyika kuanzia 8-10 Novemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Biashara cha Dubai

Akishiriki mjadala mahsusi uliojadili fursa za uwekezaji katika Sekta ya Chakula na mifumo ya uzalishaji na usambazaji chakula Bw. Gugu alisisitiza kuhusu fursa za uwekezaji Barani Afrika hususan Tanzania na jinsi Sheria Mpya ya Uwekezaji 2022 inavyolenga kuvutia uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Huduma.

Aidha, alisema kufuatia ushiriki huo ambao uliratibiwa na Shirika la AGRA na Kituo cha Kimataifa cha Biashara cha Dubai (Dubai World Trade Center), makampuni kadhaa kama vile Wirmar yameonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuweka mazingira bora na wezeshi ya ufanyaji biashara na uwekezaji.

Previous articleTGNP YAFANYA TATHMINI YA MATOKEO YA KUKUA KWA TAPO LA UFEMINIA NGAZI YA JAMII
Next articleMKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU PAMOJA NA MAWAZIRI WAELEZA MAFANIKO YA ZIARA YA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN NCHINI CHINA NA MISRI JIJINI DAR ES SALAAM 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here