Home BUSINESS WAZIRI KIJAJI AZISHAURI NCHI ZA AFRIKA KUTUMIA KISWAHILI

WAZIRI KIJAJI AZISHAURI NCHI ZA AFRIKA KUTUMIA KISWAHILI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amezihamasisha nchi za Afrika kutumia lugha ya kiswahili ili kuondoa changamoto ya lugha katika kufanya biashara ili kuleta maendeleo ya viwanda.

Aidha Waziri Kijaji amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa ili kikidhi usindani wanapotumia fursa za soko la Eneo Huru la Biashara Afrika ( AfCFTA)

Waziri Kijaji ameyasema hayo Novemba 23, 2022 wakati akishiriki katika Mkutano ngazi ya Baraza la Utendaji la Mawaziri katika Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika uliofanyika Novemba 20-25, 2022 Niamey, Niger.

Aidha, Waziri Kijaji atamwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Novemba, 2022.

Previous articleMAJALIWA AAGIZA JIJI LA DODOMA, LATRA KUKUTANA
Next articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 25-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here