Home BUSINESS WADAU WAIPONGEZA BRELA KWA UFANISI

WADAU WAIPONGEZA BRELA KWA UFANISI

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Watanzania hususani wafanyabiasha na Wajasiriamali wameshauriwa kurasimisha Biashara zao kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ili kuweza kupata fursa mbalimbali ikiwemo kuaminika katika taasi za fedha.

Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Wake-up Women’s Enterprise cha Jijini Dar es Salaam Bi. Dativa Rugalema, katika mahojiano maalum wakati wa kilele cha Maonesho ya Muungano yaliyohitimishwa Aprili 25, 2024, katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa BRELA wamekuwa msaada kwa wajasiriamali licha ya kufanya Usajili wa jina la Biashara na kukupa leseni, wamekuwa wakitoa elimu ya mambo mbalimbali yakiwemo ya Usajili wa Alama za Biashara.

“Tumeona upo umuhimu wa kusajili kwa kuwa malengo yetu ni ya muda mrefu sana Kutokana na aina ya kazi tunazozifanya.

Na kuongeza kuwa, Awali, alifikiri kuwa ili mtu uweze kusajili biashara yako BRELA ni lazima uwe na biashara kubwa lakini haiko hivyo.

Akitoa pongezi Bi. Dativa amesema, kweli BRELA ni taasisi ambayo inawalea wajasiriamali ikiwemo taasisi yake na inaendelea kuwalea kwa kuwapatia elimu amesema Bi. Rugalema.

Naye Afisa Msajili Msaidizi wa BRELA, Irene Maganga, amewapongeza wajasiriamali hao kwa kusajili jina la Kikundi chao na kuwakumbusha kuendelea kulipia ada ya kudumisha jina la Biashara kila mwaka, na kwamba kwa kufanya hivyo kutawafanya kuendelea kukua kibiashara.

BRELA waliweka kambi kwa kushiriki maonesho ya Muungano wa Tanganyika na Zanizabar yaliyofunguliwa rasmi Aprili 15 na kuhitimishwa Aprili 25, mwaka huu, katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo, Women wake up, walifanikiwa kupata usajili wa papo kwa hapo wa jina laa Biashara kutoka BRELA.

Previous articleMAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA URATIBU WA MILIKI UBUNIFU KATIKA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
Next articleMATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KISASA KUDHIBITI MAJANGA YA MIGODI YA BARRICK NCHINI YAPONGEZWA NA SERIKALI NA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA OSHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here