Home LOCAL WANANCHI WA MIPAKANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA

WANANCHI WA MIPAKANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA

Kutoka Kagera 28/9/2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametoa wito kwa wananchi waliopo katika maeneo ya mpakani mwa Uganda na Tanzania kuchukua tahadhari wakati Serikali inaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya tishio la ugonjwa wa Ebola.

Prof. Makubi ametoa wito huo leo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera, baada ya kutuma timu ya wataalam kutoka Wizara ya afya na kukutana na viongozi wa mkoa ili kujionea utayari wa kukabiliana ugonjwa huo uliotokea nchi ya jirani.

Prof. Makubi ameeleza kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hapa nchini.

Previous articleNAIBU WAZIRI MASANJA AIPONGEZA KAMATI YA KITAIFA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 65 WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI-KAMISHENI YA AFRIKA
Next articleUBALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA YATOA UFADHILI WA BILIONI 1.2 KUSAIDIA TASNIA YA UBUNIFU (SANAAPRO)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here