Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MASANJA AIPONGEZA KAMATI YA KITAIFA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 65...

NAIBU WAZIRI MASANJA AIPONGEZA KAMATI YA KITAIFA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 65 WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI-KAMISHENI YA AFRIKA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameipongeza Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani-Kamisheni ya Afrika(UNWTO) kwa kuendelea na maandalizi mazuri ili kufanikisha mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 5-7, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Gran Melia jijini Arusha.

Ameyasema hayo leo katika kikao cha tatu cha Kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa jijini Arusha.

Mhe. Masanja amewataka wanakamati hao kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha mkutano wa UNWTO unafanikiwa kwa kiwango cha juu.

“Ninaamini timu hii ni timu iliyokamilika hivyo kila mjumbe atumie uwezo wake kufanya kazi vizuri ili tusimuangushe Mheshimiwa Rais” Mhe.Masanja amesisitiza.

Ameongeza kuwa lengo la mkutano wa UNWTO ni kuitangaza Tanzania itakayosaidia kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji nchini.

Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Juma Mkomi amesema Wizara itatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha mkutano huo na pia kutatua changamoto zitakazojitokeza.

Mkutano huo utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO), Zurab Pololikashvili, Mawaziri na viongozi wenye dhamana ya kusimamia masuala ya utalii kutoka Nchi Wanachama wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kuujenga Upya Utalii Stahimilivu wa Afrika kwa Maendeleo Jumuishi ya Kiuchumi na Kijamii”

Previous articleMADIWANI HALMASHAURI YA SHINYANGA WAPITISHA TAARIFA ZA HESABU ZA MWISHO KWA MWAKA 2021/2022
Next articleWANANCHI WA MIPAKANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here