Home FASHIONS UBALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA YATOA UFADHILI WA BILIONI 1.2 KUSAIDIA TASNIA...

UBALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA YATOA UFADHILI WA BILIONI 1.2 KUSAIDIA TASNIA YA UBUNIFU (SANAAPRO)

Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Nabil Hajlaoui (kushoto), akizungumzana waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mradi wa SANAAPRO,utakaosadia tasnia ya ubunifu hapa nchini, katika hafla iliyofanyikanyumbani kwake jijini Dar es Salaa jana kutoka kulia ni MkurugenziMtendaji wa Kampuni ya Asedeva, Isack Abeneko, Mkurugenzi wa Kampuni ya FCS, Arthur Mtafya, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mudafrika,Rachel Kessi.

Mradi wa SANAAPRO ni Mradi wenye lengo la kusaidia tasnia ya ubunifu nchini Tanzania umezinduliwa leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui.

Akizindua mradi huo uliotengewa kiasi cha shiling bilioni 1.2 Balozi Nabil amesema kuwa  mradi huo ni kipaumbele cha ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania katika kusaidia Sekta ya tasnia ya ubunifu na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania na kauli ya Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron aliyoitoa katika Mkutano wa New Afrika France uliofanyika Montpelier mwezi Octoba mwaka jana.

ameeleza kuwa sekta hiyo imekuwa na mikakati ya kuvutia ili kuongeza ushindani, tija , ajira na ukuaji endelevu wa uchumi.
“Hakika ni uhai wa uchumi wa ubunifu zaidi ya hayo inatumiwa mara nyingi zaidi kukuza utangamano wa kijamii, maadili ya kijamii, ukuzaji wa kitamadubi na kama chanzo cha habari na maarifa,”amesema na kuongeza mradi huo ni kipaumbele cha Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.
“Hiyo inatokana na kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu sekta ya tasnia ya ubunifu , lakini pia katika mabadilishano ya wazi yaliyofanywa kati ya vijana wanaoshiriki sanaa na Rais Macron kwenye mkutano wa New Africa France uliofanyika Montpeller Oktoba mwaka 2021,”amesema.

Katika tukio hilo Tanzania iliwakilishwa na watu 16 kutoka kundi la wajasiriamali, viongozi kutoka mashirika ya kiraia na mabingwa wa michezo

Mradi wa SANAAPRO utakuwa na malengo kuratibu mafunzo kwa wasanii 72, uzalishaji wa filamu fupi 2 za kiwango cha ubora wa kimataifa, mafunzo kwa mafundi 70 kwenye (sauti, mwanga na usimamizi),mijadala kuhusu sekta ya ubunifu, matukio 5 ya ngoma ya kisasa ya umma na uwekezaji wa vifaa vya pamoja kwa mashirika 4 yakitamaduni.

Previous articleWANANCHI WA MIPAKANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA
Next articleMCHEZO WA KUVUTA KAMBA KIVUTIO KIKUBWA KATIKA MICHEZO YA BANDARI MOROGORO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here