Home BUSINESS TANZANIA, VIETNAM ZAWEKA MIKAKATI YA KUONGEZA THAMANI NA UZALISHAJI WA ZAO LA...

TANZANIA, VIETNAM ZAWEKA MIKAKATI YA KUONGEZA THAMANI NA UZALISHAJI WA ZAO LA KOROSHO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Revocatus Rashel (wa pili kushoto) akiwa katika jopo pamoja na vingozi wengine wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano maalumu unaoendeleza mahusiano kati ya nchi za Tanzania na Vietnam uliolenga kuitisha mitaji kutoka kwa wafanyabiashara wa Vietnam katika zao la korosho. (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje EPZA Charles Itembe (katikati) ni Balozi wa Vietnam Tanzania. Nguyen Nam Tien. kutoka kulia (wa kwanza) ni Norbert Kalembwe Meneja wa Bandari ya Mtwara, na (wapili kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Korosho Francis Alfred.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Revocatus Rashel akifuatilia mkutano huo.

Katibu tawala Mkoa Wa Mtwara Abdallah M. Malela akitoa mada katika mkutano huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje EPZA Charles Itembe akizungumza kwenye Mahojiano maalum na alipohojiwa na Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Rehema Sebabili leo Julai 21,2022 Jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka TIC Robetha Makinda (kulia) akifuatilia mkutano huo. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)


PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Katika kuhakikisha wigo wa masoko katika zao la Korosho unatanuka katika mataifa mbalimbali Duniani, Serikali ya Tanzania imeweka mikakati kuhakikisha zao hilo linaendelea kufanya vizuri katika soko la Dunia kwa kuongeza uzalishaji wa tani laki 4 katika msimu ujao wa kilimo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Revocatus Rashel katika kongamano la siku moja la kukuza soko la zao la korosho lililofanyika leo Julai 21,2023 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Ubalozi Vietnam.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa nchi ya Tanzania imeweka malengo makubwa katika uzalishaji wa zao hilo na kwamba kwa kushirikiana na Ubalozi wa Vietnam wanatarajia kuzalisha tani la 4 za korosho zilizochakatwa katika msimu ujao wa kilimo lengo likiwa ni kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza tanzania katika viwanda vya ubanguaji korosho na kupata bidhaa zilizochakatwa ili kupanua wigo wa masoko ya nje.

“Sisi kama Kituo cha Uwekezaji tumeshirikiana katika kuandaa Kongamano hili ambapo tumeliandaa katika njia mbili, moja ni wadau wanakuja hapa, na kwa pamoja tunazungumzia maeneo na vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye sekta hii ya kilimo hasa kwenye kilimo cha Korosho na uongezaji wa thamani wa zao hilo”

“Korosho ni zao la kimkakati kwa sasa, na Tanzania inazalisha kiasi cha tani laki 250 kwa mwaka lakini mkakati uliowekwa na Serikali ni kuongeza uzalishaji wa zao hilo, na sasa tumeweka lengo la kuzalisha hadi tani laki 4 kwa msimu ujao” amesema Rashel.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred amesema kuwa lengo ni kushawishi wawekezaji kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani katika zao hilo hapa nchini ili Tanzania iwe na uwezo wa kuuza korosho katika masoko mengine ya America na ulaya hali itakayosaidia kutengeneza fursa nyingi za ajira.

“Kupitia Kongamano hili la leo tunapata fursa ya kuongea na wenzetu wa Vietnam kwamba pamoja kuwa wao ndio wanunuzi wakubwa wa korosho ghafi lakini tunataka kuwaomba sasa waje kuwekeza viwanda hapa Tanzania vya kubangua korosho badala ya kununua zikiwa ghafi kwenda kubangua kwao, basi wazibangue hapa vivyo kongamano hili lliloandaliwa na Vietnam pamoja na TIC lina maana kubwa sana katika zao la korosho” amesema Alfred.

Previous articleWAZIRI NDUMBARO AZINDUA KIKOSI KAZI CHA ULINZI KWA WATOTO DHIDI YA BIASHARA YA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU JIJINI DAR
Next articleCCM YAFURAHIA UWEKEZAJI MKUBWA UNAOFANYWA NA SERIKALI KATIKA SEKTA YA ELIMU NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here