Home BUSINESS TANPAC YAWANOA MAAFISA UGANI ZAIDI YA 1000 MAPAMBANO DHINI YA SUMU KIVU

TANPAC YAWANOA MAAFISA UGANI ZAIDI YA 1000 MAPAMBANO DHINI YA SUMU KIVU

Na: Andrew Chale, Sabasaba.

SERIKALI kupitia Mradi wa Kuzuia Sumu Kuvu wa ‘Tanzania initiative for preventing aflatoxin contamination’ (TANIPA) wa Wizara ya Kilimo umeweza kufikia lengo na kwa kutoa mafunzo kwa maafisa ugani 1351 Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Kimataifa ya biashara ya 46, maarufu Sabasaba, Mtaalamu wa Sayansi ya chakula kutoka Idara ya Usalama wa Chakula, Wizara ya Kilimo, Bi. Mercy Butta alisema mradi huo awali  walipanga kutoa mafunzo kwa maafisa ugani 669,  lakini waliweza kuvuka lengo na kuwafikia zaidi.

“Mpaka sasa tumeshatoa mafunzo kwa maafisa 1351 kwa Tanzania nzima, hii ni hatua kubwa katika kuongeza juhudi za kuelimisha kutokana na tatizo kuwa kubwa, Alisema Bi. Mercy.

Na kuongeza kuwa, mradi huo wa TANIPAC ni ambao ulianza rasmi, 2019, na kutarajiwa kufikia tamati 2024, umetengewa kiasi cha Bilioni 80, kwa msaada wa fedha za Serikali ya Tanzania, Benki ya Maendeleo ya Afrika na wadau wengine 

Ambapo lengo kuu la mradi huo, kuelimisha jamii kuhusiana na athari za sumu na udhibiti wake.

Hadi sasa umekuw na msaada mkubwa kwa jamii hasa wakulima na Wafugaji”

Aidha, kwa sasa upo katika Halmashauri 18 ambazo ni Halmashauri ya Itirima, Buchosa, Bukombe, Kasulu, Kibondo, Urambo, Wilaya ya Nzega, Bahi, Kongwa, Chamba, Babati, Kiteto, Kilosa, Gairo, Nanyumbu, Namtumbo na Newara kwa upande wa Zanzibar ni  Unguja na pemba.

Hata hivyo, amesema tokea kuanza kwa mradi, mwaka 2019, wameweza  kuwafundisha wakulima 61,410 kuhusiana na udhibiti wa ubora wa mazao baada ya mavuno, lengo lilikuwa kuwafikia 60,000, ila wamepitiliza lengo hilo,

Kwa sasa hivi tunajipanga kwenda tena kuwapa elimu ya kabla ya kuvuna, tunaamini wakiwa na uelewa wa kutosha tunaweza kulidhibiti tatizo hili.” amesema  Mercy

Mradi huu ni baada ya mwaka 2016 kuwepo kwa watu walithibitika kwamba walipoteza maisha kwa sababu ya kula chakula kilichokuwa kimechafuliwa kwa kiwango kikubwa na sumukuvu, wengine waliugua kwa muda mrefu, kutokana na tatizo hilo serikali iliamua kuja na mradi huu.” Alimalizia Bi. Mercy

Previous articleSIMBA GAS YAJIWEKA TAYARI KWA UCHIMBAJI WA GESI YA UKAA BAADA YA KUPOKEA RIPOTI YA UTAFITI KUTOKA UDSM
Next articleELIMU MATUMIZI SAHIHI UTUMIAJI CHANDARUA CHA MBU YATOLEWA KWA WAKAZI WAPYA MSOMERA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here