Home Uncategorized PICHICHITURBANS KUHAMASISHA UTALII STARA FASHION WEEK

PICHICHITURBANS KUHAMASISHA UTALII STARA FASHION WEEK

 


NA: MWANDISHI WETU

STARA Fashion Week ni moja ya tamasha linalochangia ukuaji wa tasnia ya mitindo kwa kasi na kuibua wabunifu  wachanga na kutoa frusa kwa wabunifu wakongwe hapa nchin.

Huu ni msimu wa nane toka kuanziashwa kwa jukwaa hili linafanyika mara moja kwa mwaka limejikita zaidi katika mavazi ya heshima.

Mwaka huu tamasha hili litafanyika Julai 1 hadi 2 kuelekea katika msimu huu ukurasa huu umefanikiwa kufanya mahojiano na mbunifu Said Hasan Ndee ‘Pichichiturbans,’ aliyepata tuzo ya mbunifu bora wa mwaka 2021.

Anasema alianza kujihusisha na ubunifu wa mavazi akiwa chuo cha biashara CBE jijini Dar es Salaam, baada ya kusifiwa na wanafunzi wenzake kutokana na muonekano wake wa mavazi.

“Nimekulia Ilala mtaa wa Arusha jirani na nyumbani kulikuwa na sehemu ya kupiga pasi ambapo wauza mitumba walikuwa wanakuja kunyoosha nguo zao nikawa naenda kuangalia mashati na nunua kwa bei rahisi ndomana chuo walikuwa wanaona navaa vizuri,” anasema Said Hasan.

Aendelea kwa kusema baada ya kupata sifa nyingi chuo aliamua kuanza biashara ya kuuza nguo alikuwa akinunu mashati anamechisha na tai anaweka kwenye mfuko anapeleka kuuza chuoni.

Anasema baada ya muda biashara yake ilizidi kutanuka akaanza kuuzia na walimu wa chuoni hapo na kusambaza katika vyuo vya jirani IFM na DIT.


“Nilianza kupata umaarufu chuoni kwa kuvalisha walimu na wanafunzi nikanza kupata oda kutoka vyuo vya jirani ikabidi ni nunue usafiri wa pikipiki aina ya Vespa ili iwe rahisi kusambaza nguo.”

Baada ya kumaliza chuo alipata kazi katika kampuni moja akaacha kabisa kufanya kazi ya kuuza nguo ila alipata matatizo akaachishwa kazi.

“Nilipata ajira sehemu nikapata changamoto nikarudi mtaani nikaanza kujitafuta sasa ila nilikuwa tayari nina damu ya mitindo kutokana na biashara yangu ya chuo,”anasema Said Hasan.

Anasema siku moja alimtembelea rafiki yake aliyekuwa na duka la nguo kariakoo kutafuta kazi rafiki yake akamuonyesha kilemba cha Mwendokasi ambacho kilikuwa kinapendwa wakati huo akamuliza unaweza kutengeneza kama hivi.

“Rafiki yangu alinipa kilemba akanambia kinapendwa sana ila mtengenezaji ni mmoja tu Tanzania nzima, nikakichukua nikaenda kujaribu nilipo mpelekea akanambia nimepatia hapa hapo akanipa milioni moja nikaanza kutengeneza oda nyingi.”

Baada ya kufanikiwa kufanya kopi ya kile kilemba aliamua kutengeneza kilemba cha kwake mwenyewe akamchukua mwanamitindo mmoja akamvalisha akapiga picha kikakubalika ilipofika mwezi wa Ramadhani akaanza kushona nguo zenye stara za kike na kiume ndipo safari yake ya ubunifu ilipo anza kwa mara ya pili.

Mahusiano yake na Zuchu

Anasema katika mwezi wa Ramadhani mwaka huu alibahatika kufanya kazi na msanii Zuhura ‘Zuchu’ kwa kumvalisha juba ambalo watu wamelipa jina la Juba la Zuchu.

“Huwa natoa stili mpya ya juba kila ifikapo mwezi wa Ramadhani mwaka huu mtu wa kwanza kuvaa Juba hilo alikuwa msanii Zuchu kwakweli nimeliuza sana.”

Wasanii wengine ambao amewahi kuwavalisha ni Khadija Kopa, Riyama Ally na Shilole.

Mbali ya wasanii pia amebahatika kuvalisha viongozi wa serekali akiwemo Mbunge wa Mchinga Salma Kikwete, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ally.

Faida na changamoto za ubunifu

Anasema amefahamiana na watu wengi kupitia kazi ya ubunifu amepata heshima ya kuingia taasisi mbalimbali na kufahamiana na viongozi wa dini na serekali.

Kupitia ubunifu wa mavazi ametoa ajira kwa vijana ambao wanamsaidia kufanya kazi katika ofisi yake iyopo kariakoo.

Pia anaendesha familia yake pamoja na kusomesha watoto kwa kazi hiyo kwa kua hana shuhuli nyengine ya kumuingizia kipato tofauti na ubunifu.

Kwa upande wachangamoto ameeleza kuwa ni ukosekanaji wa mtaji mkubwa anapata oda nyingi ila mtaji haukidhi hivyo kama kuna mdau anaweza kuwekeza ni vizuri akijitokeza kuungana nae.

Aidha amesema kazi zake zimekuwa zikiigwa sana na wabunifu wengine wa ndani na wanje ya Tanzania.

“Wabunifu wengi wanaiga kazi zangu wamekuwa wagum kujishuhulisha na wao kuwa na matoleo yao na kibaya zaidi wanaharibu jambo linalopunguza wateja ni bora kuiga ukapatia,” anasema Said Hasan.

Hali ya soko kwa sasa.

Anasema kea upande wake hali ya soko ni nzuri kwa sababu mavazi anayo tengeneza hayana ushindani ni wabunifu wachache kwa Tanzania waonao weza kutengeneza.

Aliongeza kuwa wateja wengi wanao vaa aina ya nguo anazontengeneza  wanapenda kuchukua nguo nchin Oman kutokana na malighafi wanayotumia ni nzuri.

Aidha alitoa ushauri kwa serekali na wawekezaji kutengeneza viwanda ambavyo vitazalisha malighafi nzuri za mavazi ikiwezekana washauriane na wabunifu wakati wa kutengeneza

Ujio wa Collection ya Utalii.

Anasema mwaka huu atashiriki kuonyesha mavazi kwa mara nyengine katika jukwaa la Stara fashion amepanga kufanya zaidi ya mwaka jana kwa sababu alijizolea umaarufu mkubwaa baada ya kutwaa tuzo ya mbunifu 
bora wa mwaka.

Aliongeza kuwa toleo la mwaka huu litajikita zaidi katika uhamasushaji wa utalii hapa nchin ikiwa ni hatua ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan.

“Mama yetu amefanya jambo kubwa katika sekta ya utalii na mimi kama mbunifu nimeamua kumuunga mkono kwa kutengeneza nguo ambazo zitatangaza utalii kama  ilivyo Royol Tour,” anasema Said Hasan.
Previous articlePROF. MAKUBI AKUTANA NA NA KUZUNGUMZA NA MADAKTARI BINGWA MISRI
Next articleCAMARTEC MBIONI KUANZISHA KITOVU CHA ZANA ZA KIHANDISI MKOA WA SIMIYU.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here