Home LOCAL TCRA YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI MTANDAO KUZINGATIA SHERIA, KUWA WABUNIFU WA VIPINDI

TCRA YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI MTANDAO KUZINGATIA SHERIA, KUWA WABUNIFU WA VIPINDI

 PICHA ZOTE NA: TCRA

Na: Mwandishi Wetu.

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa vyombo vya habari mtandaoni vinatakiwa kujenga uimara wake katika kutangaza maudhui ya kujenga jamiii kwa kuandaa vipindi vilivyo bora.

Akizungumza katika Semina ya siku mbili ya  Mafunzo ya Vyombo vya Habari vya Mtandaoni Mwenyikekiti wa Kamati hiyo Habbi Gunze amesema kuwa maudhui lazima yazingatie weledi na sheria kwanii vyombo hivyo ili kuleta tija kwa  jamii.

Amesema kuwa Teknolojia inakwenda kwa kasi hivyo vyombo vya habari mtandao vifanye kazi kuelimisha jamii na kuacha kuwa sehemu ya kupotosha na kwamba sheria itatumika kudhibiti hali hiyo.

“Tutakwenda pamoja katika kutoa elimu katika kuhakikisha mnasimama na matokeo yake jamii itaelimika huku maendeleo yakionekana kutokana na kupata habari zinajenga zaidi” amesema Gunze

Mjumbe wa Kamati ya Maudhui wa TCRA Dereck Mrusuri amesema kuwa vyombo vya habari mtandao vinatakiwa kubadilisha mtazamo wa kufanya kazi hiyo kwa kuwa na vipindi vinavyojenga na hatimae kuwa na uwezo wa kifedha na kujiendesha.

Amesema kuwa kuna watu wamefanikiwa vizuri katika kutengeneza vipindi vinavyojenga na jamii ikafuata na kupata mabadiliko ya kiuchumi kutokana na chombo cha habari kujikita katika kutatua changamoto ndani ya jamii.


Mrusuri amesema kuwa katika kufanya hivyo ni kuongeza ubunifu ambao watu wengine hawafanyi hivyo vyombo vya habari mtandaoni vina uwanja mpana zaidi katika eneo hilo.

Aidha amesema kuwa katika kufanya kazi kwa ustadi kwa vyombo vya habari kupitia waandishi kuzingatia masuala ya uvaaji kwani wakati mwingine mtu anaweza kudhalaulika kutokana na mavazi.

Mkuu wa Kitengo cha Leseni za Mawasiliank wa TCRA  Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuna TV za mitandaoni kazi yake kuchukua vipindi vya nje ya nchi wakati leseni yake amechukua TCRA.

Amesema kuwa vipindi vingi watu wanatumia lugha ya kiingereza wanakwenda katika kutoa elimu kutumia lugha ya kiswahili kwani kiswahili kina maneno yakwenda kukidhi matamanio ya watazamaji.

Semina hiyo ya siku mbili imefanya Mei 18 na 19,2022 katika ukumbi wa mikutano wa TCRA Jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na washiriki zaidi ya 100 wakiwemo washiriki kwa njia ya mtandao kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Previous articleNMB FAUNDATION YATANGAZA UFADHILI ELIMU KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU
Next articleRAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKOA WA TABORA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here