Home BUSINESS NMB FAUNDATION YATANGAZA UFADHILI ELIMU KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU...

NMB FAUNDATION YATANGAZA UFADHILI ELIMU KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Foundation, Ruth Zaipuna (wa pili kushoto), akizindua rasmi dirisha la kupokea maombi ya ufadhili wa wanafunzi wanaotegemea kuingia kidato cha tano mwaka huu na wale wanaotarajia kuingia vyuo vikuu kwa ajili ya shahada ya kwanza ya masomo. Kushoto ni mjumbe wa Bodi, Juma Kimori na kulia ni Katibu wa NMB Foundation, Consolata Mosha na mjumbe wa Bodi, Filbert Mponzi.9.

Taasisi ya NMB Foundation imetangaza kuanza rasmi utaratibu wa kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kidato cha tano, sita na elimu ya juu baada ya programu hiyo kuzinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mwishoni mwa mwaka jana

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Foundation, Ruth Zaipuna amesema wameanza kupokea maombi kupitia matawi yote ya benki hiyo yaliyopo nchi nzima na tovuti ya NMB Foundation.

“Kwa kuanzia tutatoa ufadhili kwa wanafunzi 200, ambapo 150 watakuwa wa kidato cha tano na sita, wanafunzi 50 watakuwa wa elimu ya juu. Fadhili utalipia gharama zote za masomo ikiwemo ada, fedha za kujikimu, vifaa na mahitaji mengine yatakayotajwa kweye fomu ya kujiunga na shule au chuo,” amesema Ruth.

Alifafanua kuwa kwa wanfunza wa sekondari watakaopata ufadhili watalipiwa ada, nauli, vifaa vya kujifunzia, fedha za kujikimu, bima ya afya na mahitaji mengie watakayotakiwa kutoka shule. Kwa upande wa elimu ya juu, wanafunzi watalipwa ada, fedha za kujikimu, fedha za mafunzo kwavitedo, Laptop na gharama nyingine watakazotakiwa kwenye fomu ya kujiunga na chuo.

Aidha, Zaipuna alisema wamejipanga kuweka masomo ya vipaumbele kwa wanafunzi watakaopata fursa ya udhamini. Lengo ni kuhakikisha wanashiriki mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kupitia malezi na mafunzo watakayopata wanafunzi hao.“

Tutaangalia kwa kina masomo ya takwimu na mahesabu, biashara na uchumi, Teknolojia ya Mawasiliano ya Umma, uhandisi, mafuta na gesi pamoja na sayansi na teknolojia,” alibainisha Zaipuna na kuongeza:

“Nina imani kupitia programu hii tutaibua vipajij na tutatimiza ndoto za vijana. Kadiri tutakavyoendelea idadi ya wanafunzi watakaonufaika itaongezeka kulingana na mahitaji ambapo tutapanua wigo wa wadau wengine watakaotaka kushirikiana nasi kwenye jambo hili muhimu kwa maendeleo ya nchi.”

Katika hatua nyingine, Ruth alisema NMB Foundation itahakikisha watu watakaohusika kukusanya na kupitisha wanafunzi wanaofaa kwa kupewa ufadhili watakuwa makini kutimiza vigezo, ambapo kwa wale watakaokwenda kinyume na utaratibu watachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Tunataka kulifanya zoezi hili liwe na uwazi na ukweli, ndio maana tumesema tutawashirikisha hata viongozi wa serikali za mitaa kuanzia kata hadi mitaa, lengo ni kuhakikisha wanufaika watakaopatikana ni kweli wana vigezo vinavyohitajka,” alisisitiza Zaipuna.

Previous articleMANDALIZI MKUTANO WA 65 UNWTO-CAF YAANZA, DKT MICHAEL ASISITIZA WANAKAMATI KUCHUKULIA UMUHIMU NA UZITO JUKUMU WALILONALO
Next articleTCRA YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI MTANDAO KUZINGATIA SHERIA, KUWA WABUNIFU WA VIPINDI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here