Home BUSINESS SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA UFANYAJI BIASHARA NCHINI

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA UFANYAJI BIASHARA NCHINI

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji,akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania pamoja na kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

 

WAZIRI  wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji,akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright   mara baada ya kufanya mazungumzo kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania  pamoja na kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili jijini Dodoma.

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini na iko tayari kuwawezesha wawekezaji kutoka ndani na nje wenye nia ya kuwekeza nchini.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo  wakati  alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright  kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania  pamoja na kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma Aprili 05, 2022.

Akiwa ameambata na Viongozi wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara akiwemo Katibu Mkuu Prof. Godius Kahyarara, Naibu Katibu Mkuu  Bw. Ally Gugu, Dkt. Kijaji amemhakikishia Balozi huyo kuwa Serikali iko tayari kuwawezesha wawekezaji kutoka Marekani katika maeneo ya  uzalishaji wa Mbolea na mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo kama ngano, mafuta ya kula na sukari ili kuondoa upungufu uliopo nchini.

Naye Balozi huyo wa Marekani nchini Tanzania amesema Marekani itaendelea kuwekeza na kufanya biashara nchini katika maeneo ya kilimo biashara, uchumi wa blue, uchakataji wa mazao, uwezeshaji vikundi vya wanawake wajasiriamali pamoja na kuandaa maonesho na makongamano mbalimbali yanayolenga kuhamasisha na kukuza biashara nchini.

Previous articleWAZIRI UMMY AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA DENMARK DODOMA
Next articlePROF. MAKUBI ATOA WITO KWA WANANCHI KUWAHI KUFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here