Home Uncategorized MEYA JIJI LA DAR ES SALAAM AFANYA ZIARA YA KIKAZI ZAHANATI YA...

MEYA JIJI LA DAR ES SALAAM AFANYA ZIARA YA KIKAZI ZAHANATI YA KITUNDA.

 

Na: Juma Mizungu, PuguMedia.

Meya Jiji la Dar es salaam Mhe Omary Kumbilamoto amefanya ziara ya kikazi katika Zahanati ya Kitunda, Lengo la ziara hiyo ni kujionea jinsi gani ya utoaji wa huduma katika Zahanati hiyo.

Zahanati ya Kitunda ni moja ya Zahanati zinazofanya vizuri kwasasa Kitaifa na imeshika nafasi ya 3 katika utoaji wa huduma pamoja na Data kitaifa, inahudumu jumla ya Kata mbili Kitunda pamoja na Kata Mzinga inatoa huduma kwa Wananchi wapatao 80,868 katika huduma 15 ikiwemo OPD,TB,Baba Mama na Mtoto, Afya ya Akili na walio athirika na madawa ya kulevya n.k.

Zahanati hiyo kwasasa inategemea vyanzo vitano vya mapato ikiwemo Papo kwa Papo,Ruzuku kutoka Serikali (Basket Fund), Bima (NHIF & ICHF), MSD pamoja na BILATERAL PEFFAR.

Mbali na utoaji wa huduma bora Zahanati hiyo inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa wahudumu, upungufu wa majengo, Generator pamoja na ukarabati wa jengo la kichomea taka.

Mhe. Kumbilamoto amewapongeza wauguzi wote wa Zahanati ya Kitunda wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo Dkt Magreth Methew kwa kufanya vizuri katika kutoa huduma kitaifa na upande wa Data, Lakini Mhe. Kumbilamoto ameahidi kuzifanya kazi changamoto zote kwa kuanza na kukarabati jengo la kuchomea taka.

Credit – Pugu Media Online
Previous articleBRELA YAFANYA USAJILI WA MOJA KWA MOJA NA KUTOA VYETI JIJINI TANGA
Next articleDKT. GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MKOA WA IRINGA QUEEN SENDIGA JIJINI DODOMA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here