Home LOCAL DC MACHA AIPONGEZA FADev KWA KUTOA ELIMUA KWA WAANDISHI WA HABARI

DC MACHA AIPONGEZA FADev KWA KUTOA ELIMUA KWA WAANDISHI WA HABARI

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akifungua mafunzo ya waandishi wa habari.

Evans Rubara kutoka FADev akitoa mafunzo kwa waandishi wa Habari



Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo hayo.

Waandishi wahabari katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kahama pamoja na watoa Mafunzo kutoka FADev

Na,Saimon Mghendi, Kahama.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha, ameipongeza taasisi ya FADev kwa kuwapa  mafunzo waandishi wahabari yanayohusiana na sekta ya wachimbaji wadogo wa madini, Jambo ambalo litawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi wakati watakaapokua wanandika habari zinazohusiana na wachimbaji wadogo nchini.

Macha ameyasema hayo leo wakati alipokua akifungua semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari ya siku nne yalioandaliwa na taasisi ya kuendeleza wachimbaji wadogo nchini ya FADev, Katika ukumbi wa Hoteli ya Submarine katika Manispaa ya Kahama.

Mafunzo hayo ya siku nne yanayotolewa na taasisi ya FADev kwa waandishi wa habari, yanajumuisha waandishi wa habari wa kutoka mikoa mitatu, ambayo ni Shinyanga,Geita pamoja na Mwanza.

 

Previous articleRAIS MHE.SAMIA SULUHU ASHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI NAMNA KUOKOA UCHUMI NA KUKABILIANA NA KORONA
Next articleMWAKANG’ATA ALILIA UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA MJINI ATAKA SERIKALI ICHUKUE HATUA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here