Home LOCAL MWAKANG’ATA ALILIA UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA MJINI ATAKA SERIKALI ICHUKUE HATUA

MWAKANG’ATA ALILIA UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA MJINI ATAKA SERIKALI ICHUKUE HATUA

Na: Khalfan Akida, DODOMA

Serikali imeshauriwa kuuntengeneza upya uwanja wa ndege wa Sumbawanga Mjini kwa viwango bora ili kufungua milango kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika mkoa wa Rukwa.

Hayo yamesemwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Rukwa, Mhe. Bupe Mwakang’ata wakati akichangia hotuba ya bajeti wizara ya Ujenzi na uchukuzi leo bungeni jijini Dodoma.

“tunashukuru serikali iliwalipa wakazi waliopo karibu na uwanja wa ndege Sumbawanga lakini baada ya hapo hali imekuwa ni kimya kabisa, ni miaka mine sasa imepita tunapitisha bajeti ya uwanja wa Ndege Sumbawanga”

Katika mchango wake, Mhe. Bupe amesema serikali inapaswa kuchukua hatua ya kuukarabati uwanja wa ndege wa Rukwa kutokana na fursa nyingi zilizopo mkoani humo.

“kuna madini, mazao, vivutio vya utalii hivyo mhe. Waziri atakapokuja atueleze uwanja wa Ndege utajengwa lini”

Katika hatua nyingine Mhe. Bupe ameitaka serikali kuijenga kwa lami barabara inayotoka Kibaoni mpaka Mloho kutokana na serikali kutumia fedha nyingi kuikarabati mara kwa mara kwa sababu ya uharibifu unaojiotekeza wakati wa mvua.

Mhe. Bupe amesema barabara hiyo ni muhimu kwa mkoa wa Rukwa kwa sababu inapatikana katika bonde la Rukwa ambapo ndio sehemu kubwa yanapotoka mazao ya chakula na biashara mkoani humo.

“barabara hii ni ya kiuchumi kwa sababu inapita katika bonde la Rukwa ambako ndiko wakulima wanalima mazao ya biashara na chakula hivyo ijengwe kwa lami kuokoa ukarabati wa mara kwa mara

Aidha Mhe. Bupe ameishauri serikali kuangalia upya changamoto za ucheleweshwaji wa malipo kwa wakandarasi wa miradi mbalimbali hadi kupelekea wakandarasi hao kufungiwa biashara zao kuwa sababu ya madeni.

“wakandarasi wanalalamika sana wanapokuwa wamefanya kazi wanacheleweshewa sana pesa zao, lakini kabla ya kufanya kazi wanakatwa pesa zao na kupelekea wanafungiwa biashara zao”

Previous articleDC MACHA AIPONGEZA FADev KWA KUTOA ELIMUA KWA WAANDISHI WA HABARI
Next articleSHULE YA BILIONEA LAIZER YAKABILIWA NA UHABA WA WALIMU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here