Na: Saimon Mghendi, KAHAMA.
Wafanyabiashara wa nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Kongo DRC, wametakiwa kuitumia bandari ya nchi kavu ya Isaka iliyopo, Mkoa wa kikodi wa Kahama, kwa kuzingatia taratibu za sheria za forodha zinazowekwa na mamlaka ya mapato nchini TRA, ili kuboresha mfumo thabiti wa kibiashara kwa ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara SADC.
Kaimu meneja wa TRA Mkoa wa kikodi kahama, Irene Hans, Ameyasema hayo Wakati Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye uzinduizi wa maonesho ya wiki moja ya wajasiriamali kutoka Mikoa tofauti hapa nchini yanayofanyika katika manispaa ya kahama, Mkoani Shinyanga, Yaliyo andaliwa kwa ushirikiano wa kampuni ya GS1 na kituo cha baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Tanzania, kilichopo chini ya ofisi ya waziri Mkuu, bunge, sera, kazi, vijana na watu wenye ulemavu kitawashirikisha wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali zaidi ya 230
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, amesema serikali imeandaa mazingira mazuri ya huduma kwa wananchi kwa kuweka ofisi zenye mahitaji muhimu eneo moja.
Nao baadhi ya Wajasiriamali wamewapongeza waandaaji wa maonesho hayo na kusema kuwa yatawasaidia kunadi biashara bidhaa zao.