Home BUSINESS WAKULIMA 40,000 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA UDONGO NA MAFUNZO YA KILIMO CHENYE...

WAKULIMA 40,000 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA UDONGO NA MAFUNZO YA KILIMO CHENYE TIJA.


NA: MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Kalambo, mkoa wa Rukwa, Kalolius Misungwi, amezindua mafunzo ya kilimo chenye tija yanayotolewa na kampuni ya OCP Afrika msimu wa pili Sumbawanga mjini.

OCP Afrika kupitia kampuni tanzu ya OCP Tanzania  ilizindua awamu ya kwanza mradi wa tathimini ya udongo mwaka 2019, na awamu hii ya pili ya mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakulima na wadau wa kilimo wa mikoa ya Rukwa, Morogoro, Mbeya na Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Idara za Kilimo (taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) kituo cha Uyole), tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI). Mradi wa OCP SCHOOL LAB Utatoa ushauri sahihi kwa mkulima mmoja mmoja na mapendekezo yanayolenga kuongeza  tija ya  mazao kama mahindi, mpunga, viazi pamoja na alizeti. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Ndugu Joseph Mkirikiti,  Mkuu wa wilaya ya Kalambo, Kalolius Misugwi alisema, sekta ya kilimo imeajiri asilimia 65%ya watanzania wote.

“Sekta ya kilimo nchin ni imetoa ajira kwa kiasi kikubwa pia imelihakikishia taifa upatikanaji wa chakula kwa asilimia 100% pamoja na malighafi za viwandani, lakini bado idadi hiyo ya watanzania wanao jishughulisha na  kilimo haipo katika uwiano sawa na idadi ya watanzania wote  kwa sababu ya tija ndogo inayotokana na uzalishaji mazao, mpango huu utasaidia kuongeza na tija na bila shaka kuongeza uzaishaji wa mazao ya kilimo” anasema Misungwi.

Kwabupande wa Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya OCP Tanzania Dkt. Mshindo Msolla alisema, kampuni hiyo ikishirikiana na Serikali imeandaa mchakato wa upimaji wa udongo kwa zaidi ya vijiji 100 ndani ya mkoa wa Rukwa. 

“Lengo ni kuwaelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila gharama zozote kwa wakulima hao majibu yatatolewa kwao pamoja na ushauri wa kitaalamu juu ya nini kifanyike ili kutunza ubora wa udongo wa kijiji husika kwa matokeo bora ya shughuli za kilimo, katika kila kijiji zaidi ya wakulima 100 watafikiwa na kuelimishwa namna bora za kufanya kilimo kiwe cha mahindi, mpunga au alizeti kulingana na maeneo waliopo.”

Aliongeza kuwa kwa mradi huu una tazamia kufikia wakulima 10,000 kwa mkoa wa Rukwa pekee kwakipindi cha  mwaka huu.

Previous articleBRELA YAALIKWA BUNGENI KUSHUHUDIA BAJETI YA WIZARA YAO IKISOMWA.
Next articleTRA KAHAMA YAWAASA WAFANYABIASHARA BIASHARA WA NCHI JIRANI KUZINGATIA TARATIBU ZA KISHERIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here