Home BUSINESS TRA KAHAMA YAWAASA WAFANYABIASHARA BIASHARA WA NCHI JIRANI KUZINGATIA TARATIBU ZA KISHERIA

TRA KAHAMA YAWAASA WAFANYABIASHARA BIASHARA WA NCHI JIRANI KUZINGATIA TARATIBU ZA KISHERIA

 

Na: Saimon Mghendi, KAHAMA.

Wafanyabiashara wa nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Kongo DRC, wametakiwa kuitumia bandari ya nchi kavu ya Isaka iliyopo, Mkoa wa kikodi wa Kahama, kwa kuzingatia taratibu za sheria za forodha zinazowekwa na mamlaka ya mapato nchini TRA, ili  kuboresha mfumo thabiti wa kibiashara kwa ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara SADC.

Kaimu meneja wa TRA Mkoa wa kikodi kahama,  Irene Hans, Ameyasema hayo Wakati Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye uzinduizi wa maonesho ya wiki moja ya wajasiriamali kutoka Mikoa tofauti hapa nchini yanayofanyika katika manispaa ya kahama, Mkoani Shinyanga, Yaliyo andaliwa kwa ushirikiano wa kampuni ya GS1 na kituo cha baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Tanzania, kilichopo chini ya ofisi ya waziri Mkuu, bunge, sera, kazi, vijana na watu wenye ulemavu kitawashirikisha wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali zaidi ya 230

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, amesema serikali imeandaa mazingira mazuri ya huduma kwa wananchi kwa kuweka ofisi zenye mahitaji muhimu eneo moja.

Nao baadhi ya Wajasiriamali wamewapongeza waandaaji wa maonesho hayo na kusema kuwa yatawasaidia kunadi biashara bidhaa zao.

Previous articleWAKULIMA 40,000 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA UDONGO NA MAFUNZO YA KILIMO CHENYE TIJA.
Next articleWIZARA YA AFYA YAANZA UTEKELEZAJI WA MABORESHO YA HUDUMA ZA MATIBABU KWA WAZEE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here