Home BUSINESS MITAALA IZINGATIE MABADILIKO YA KIUCHUMI NA TEKNOLOJI-MAJALIWA

MITAALA IZINGATIE MABADILIKO YA KIUCHUMI NA TEKNOLOJI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kuwa mitaala inayoandaliwa ihakikishe inazingatia mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo ya kiteknolojia.

Amesema hayo leo (Ijumaa, Novemba 22, 2024) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la tano la Maendeleo ya Biashara na Uchumi linalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma.

Amesema kuwa kuna umuhimu wa kutumia teknolojia katika kuboresha elimu ya biashara kwa kutumia jukwaa la mtandao kutoa mafunzo ya biashara, matumizi ya programu za kisasa za biashara, na kupanua matumizi ya teknolojia katika biashara na ujasiriamali. “Hivyo, nitoe rai kwa taasisi za elimu na mafunzo ya biashara kujikita katika matumizi ya teknolojia katika utoaji wa mafunzo”

Pia, ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau waendelee kuimarisha na kuboresha mifumo ya elimu ya biashara katika ngazi zote za shule na vyuo na kuhakikisha inakidhi mahitaji ya soko la ajira.

Katika Hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka Taasisi za elimu na mafunzo ya biashara zihakikishe zinakuza ushirikiano na sekta binafsi ili kusaidia katika kubaini mahitaji halisi ya soko na kutoa mafunzo na elimu inayoendana na mabadiliko ya sekta ya biashara.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni muhimu kuhakikisha kuwa biashara si tu zinanufaisha wamiliki, bali pia zinachangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. “Biashara zinapaswa kuchangia katika kulinda mazingira na ustawi wa jamii”.

Kw upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amesema kuwa kongamano hilo maalum la kitafiti litasaidia kuibua mijadala itakayowezesha kubaini changamoto na fursa zitazoisaidia nchi kupata mafanikio katika sekta ya biashara na uchumi.

“Kwa takwimu za mwaka 2001 vijana waliomaliza vyuo vikuu, walikuwa 51800, na kadiri miaka inavyoenda ndivyo wanavyoongezeka, Serikali pekee haiwezi kuajiri, tunategemea wengine waende sekta binafsi, tunazo fursa za masoko kwenye nchi za SADC, Afrika Mashariki, na la huru za afrika; ili kuweza kuyafikia masoko hayo lazima tufanye tafiti”

Naye, Mkuu wa chuo cha Elimu ya Biashara Prof. Edda Tandi Lwoga, amesema kuwa wamefanikiwa kuongeza bajeti ya utafiti kutoka milioni 46 mwaka 2018 hadi milioni 300 mwaka wa fedha 2023/2024.

“kipindi cha miaka mitano, Chuo kimefanikiwa kuchapisha jumla ya machapisho 288 katika majarida ya kitaifa na kimataifa, kutokana na juhudi za wahadhiri na watafiti wetu katika kuendeleza elimu na kuzalisha maarifa mapya”.








Previous articleMNEC ASSAS AELEZA MKAKATI WA CCM KATIKA VITUO 87,000 VYA KUPIGA KURA
Next articleUMMY MWALIMU HAPOI, AENDELEA KUWAOMBEA KURA WAGOMBEA WA CCM UCHAGUZI S/MITAA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here