AFISA MTENDAJI wa Kata ya Liwiti Ignas Maembe mepiga marufuku Wenyenyumba wa Kata ya Liwiti na Madalali kupangisha wapangaji lazima wasajilie katika datfari la makazi.
AFISA MTENDAJI Iginas alisema hayo Dar es Salaam juzi wakati wa kikao cha Wananchi wa Mtaa wa Liwiti alipokabidhi Daftari waraka wa utekelezaji wa maelekezo kuhusu Ulinzi na Usalama ngazi ya Kaya na Mtaa.
“Naagiza Marufuku Wenyenyumba na madalali wapangisha mpangaji lazima asajiliwe Daftari la makazi taarifa za mpangaji ziwepo.alisema Maembe .
Maembe alisema kila mpangaji kuakikisha anasajiliwa katika Mtaa Kama sheria ya Serikali za Mtaa ya mwaka 1982 za Mitaa mamlaka na miji
Maembe alisema kuwa Wenyeviti wanatakiwa kuhakikisha wanawatambua wakazi wao pamoja na kuwabaini wapangaji wapya wanaomia katika mtaa kwa kutoa taarifa Serikali za Mitaa au kwa AFISA MTENDAJI wa Kata.
Pia kuamasisha wananchi kushiriki katika Ulinzi ns Usalama ikiwemo kuchangia gharama Ulinzi kwa kufuata taratibu zilizopo katika Mtaa.
Aidha pia aliwataka wenye nyumba kuweka taa nje kwa ajili ya Usalama wa Mali zao
Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana pamoja kwa kusaidia kutoa taarifa sahihi katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakama
Aliwataka Wamiliki wa nyumba wawe na mikataba maalum wanakuwa na mikataba inayotambulika kwa ajili ya kupangisha nyumba zao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Tabata Mrakibu wa Polisi Colle Senkondo aliwataka wakazi wa Liwiti kushirikiana na Jeshi la Polisi ikiwemo kuunda Ulinzi Shirikishi.
Kamanda Senkondo alisema aliwataka wazazi wawafichue vijana wao wahalifu waache kujiusisha na vitendo viovu.
Mwisho