Home LOCAL MTENDAJI LIWITI, APIGA MARUFUKU MADALI,WENYUMBA KUPANGISHA LAZIMA WAPANGAJI WASAJILIWE...

MTENDAJI LIWITI, APIGA MARUFUKU MADALI,WENYUMBA KUPANGISHA LAZIMA WAPANGAJI WASAJILIWE DAFTARI LA MAKAZI.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Liwiti Ignas Maembe akikabidhi Waraka kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata  Mrakibu wa Polisi College Senkondo ,Waraka wamekabidhi kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa   utekelezaji maelekezo ya Serikali kuhusu Ulinzi na Usalama ngazi ya Kaya na Mtaa ambapo Wapangaji wote wanatakiwa wajiandikishe katika daftati LA makazi  (PICHA Na HERI SHAABAN).

Afisa Mtendaji wa Kata ya Liwiti Ignas Maembe akikabidhi Waraka Diwani wa Kata ya ya Liwiti Alice Mwangomo ,Waraka wamekabidhi kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa   utekelezaji maelekezo ya Serikali kuhusu Ulinzi na Usalama ngazi ya Kaya na Mtaa ambapo Wapangaji wote wanatakiwa wajiandikishe katika daftati LA makazi  (PICHA Na HERI SHAABAN).

Mjumbe wa Serikali za Mtaa LIWITI Neema Mkiwa akiwaonyesha wananchi wake Daftari la makazi ambalo linatakiwa kujioresha wageni wote wanaoingia ndani ya Liwiti ,(PICHA NA HERI SHAABAN).


Na: Kheri Shaaban, DAR ES SALAAM.

AFISA MTENDAJI wa Kata ya Liwiti Ignas Maembe mepiga marufuku  Wenyenyumba wa Kata ya Liwiti na Madalali  kupangisha wapangaji lazima wasajilie katika datfari la makazi.

AFISA MTENDAJI Iginas  alisema hayo Dar es Salaam juzi wakati wa kikao cha Wananchi wa Mtaa wa Liwiti alipokabidhi Daftari waraka wa utekelezaji wa maelekezo kuhusu Ulinzi na Usalama ngazi ya Kaya na Mtaa.

“Naagiza Marufuku Wenyenyumba na madalali wapangisha mpangaji lazima asajiliwe Daftari la makazi taarifa za mpangaji ziwepo.alisema Maembe .

Maembe alisema kila mpangaji kuakikisha anasajiliwa katika Mtaa Kama sheria ya Serikali za Mtaa ya mwaka 1982 za Mitaa mamlaka na miji

Maembe alisema kuwa Wenyeviti wanatakiwa kuhakikisha wanawatambua wakazi wao pamoja na kuwabaini wapangaji wapya wanaomia katika mtaa kwa kutoa taarifa Serikali za Mitaa au kwa AFISA MTENDAJI wa Kata.

Pia kuamasisha wananchi kushiriki katika Ulinzi ns Usalama ikiwemo kuchangia gharama Ulinzi kwa kufuata taratibu zilizopo katika Mtaa.

Aidha pia aliwataka wenye nyumba kuweka taa nje kwa ajili ya Usalama wa Mali zao 

Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana pamoja kwa kusaidia kutoa taarifa sahihi katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakama

Aliwataka Wamiliki wa nyumba wawe na mikataba maalum wanakuwa na mikataba inayotambulika kwa ajili ya kupangisha nyumba zao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Tabata Mrakibu wa Polisi Colle Senkondo aliwataka wakazi wa Liwiti kushirikiana na Jeshi la Polisi ikiwemo kuunda Ulinzi Shirikishi.

Kamanda Senkondo alisema aliwataka  wazazi wawafichue vijana wao wahalifu waache kujiusisha na vitendo viovu.

Mwisho

Previous articleUZINDUZI WA ALBAMU MBILI ZA MAMAJUSI ANGLIKANA MOSHI, ZAIDI YA MILIONI NANE ZAPATIKANA INJILI YAENEZWA
Next articleACT WAZALENDO WAMLILIA PROF. BAREGU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here