Home BUSINESS BOT YAUPIGA MWINGI MAONESHO YA SABASABA.

BOT YAUPIGA MWINGI MAONESHO YA SABASABA.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imenyakua makombe mawili kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45, moja likiwa la Mshindi wa Tatu wa Jumla na lingine likiwa la Mshindi wa Kwanza kwa Taasisi.

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dkt. Bernard Kibesse, akipokea zawadi ya kombe baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupata Ushindi wa tatu wa jumla katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.


Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dkt. Bernard Kibesse, akielezea jambo kwa wataalam wa BoT kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha pamoja na Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, kwenye banda la BoT Sabasaba.

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dkt. Bernard Kibesse, akifafanua jambo kwa wataalam wa BoT kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha,  kwenye banda la BoT Sabasaba.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni Afisa Rasimali Watu Mwandamizi, akijadili jambo na Bi. Consolata Shao,  kwenye banda la BoT Sabasaba.

Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Missango, akipewa maelezo kuhusu Dhamana za Serikali na Mchambuzi wa Masuala ya Fedha, Bw. Martin Kalihose,  kwenye banda la BoT Sabasaba.
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina, akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa BoT, Bw. Benard Dadi, katika majadiliano na Mchambuzi wa Mifumo, Bw. Robert Masalu na Mchambuzi wa Fedha Mwandamizi, Bi. Kidee Mshihiri 

Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani BoT, Bi. Aziza Hamis (kulia) akipewa maelezo kuhusu Maendeleo ya Uchumi wa Tanzania na Mchumi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bi. Sylvia Bwakea. 

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo ya TEHAMA, Bw. Joel Ngussa, Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha, Bw. Alexander Ng’winamila, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Missango, Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Jamhuri Ngelime, Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, Bw. Augustino Hotay, Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu, Bw. Nixon Kyando na Afisa Benki Mkuu Mwandamizi, Bi. Restituta Minja  kwenye banda la BoT Sabasaba.
Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bw. Richard Malisa (kushoto) akijadiliana jambo na Afisa Rasimali Watu Mwandamizi, Bi. Joyce Shala na Afisa Benki, Bi. Rukia Muhaji. 
 
 
Previous articleNAIBU WAZIRI BYABATO: MRADI WA UMEME WA (JNHPP) UTAMALIZA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI
Next articleUJENZI MJI WA SERIKALI MTUMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here