Home Uncategorized NAIBU WAZIRI BYABATO: MRADI WA UMEME WA (JNHPP) UTAMALIZA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI...

NAIBU WAZIRI BYABATO: MRADI WA UMEME WA (JNHPP) UTAMALIZA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI

Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato  akimsikiliza Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wakati alipokuwa akielezea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power unaojengwa Rufiji katika mikoa ya Pwani na Morogoro wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TANESCO  katika maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato  akihoji jambo kwa Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wakati alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi huyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaojengwa Rufiji katika mikoa ya  Pwani na Morogoro wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TANESCO  katika maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato  akimsikiliza Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wakati alipokuwa akimfafanulia zaidi  maendeleo ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power unaojengwa Rufiji katika mikoa ya Pwani na Morogoro  wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TANESCO  katika maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

 Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato  akimsikiliza Bw. Agustine Kasale afisa Mawasiliano Kampuni ya Uendelezaji Joto Ardhi Tanzania (TGDC) wakati alipotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato  akimsikiliza Mhandisi wa Mitambo kutoka Shirika la (TGDC) kwenye  maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

 Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato  akioneshwa mtambo uliobuniwa na Amani Christopher Mhandisi wa Mitambo kutoka Shirika la (TGDC) kwenye  maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato amesema Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project JNHPP unakwenda kutatua changamoto nyingi za maendeleo kwa watanzania katika suala zima la upatikanaji wa umeme wa Uhakika.

Naibu Waziri Byabato ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la TANESCO kwenye  maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 06, 2021 na kujionea ubunifu wa wahandisi watanzania ambao wamebuni mfano wa mradi huo na kuuleta kwenye  maonesho hayo kwa ajili ya kuwaonesha wananchi kile kinachoendelea huko Rufiji.

Amesema kwa sasa tunazalisha Megawati moja ya umeme wa maji kwa shilingi 36 wakati umeme wa mafuta tunazalisha megawati moja kwa zaidi ya shilingi 500 hivyo utaona kabisa kuwa umeme wa maji ni wa bei rahisi kabisa.

“Na ndiyo maana umeme wa  vijijini kwa sasa kuunganisha ni shilingi elfu 27.000 tu kitu ambacho kinarahisisha maisha ya watanzania  kwa sababu umeme ndiyo kila kitu katika maendeleo,”. amesema Waziri Byabato.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kauli mbiu yake ya “Kazi Iendelee” hii inamaanisha kwamba mradi huu wa umeme ni muhimu na utaliletea taifa faida kubwa katika suala zima la maendeleo ya viwanda.

Amesema kukamilika kwa bwawa hili itakuwa ni faraja kubwa kwa sababu faida za mradi huu tutakuwa tumeongeza umeme wa gharama na nfuu kwa watanzania na  kwa majirani zetu hapa nchini na usambazaji wa umeme kwa vijijini Rea itakuwa chini kabisa.

Previous articleDKT.GWAJIMA AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TARATIBU WAKATI WA KUCHUKUA MIILI YA MAREHEMU
Next articleBOT YAUPIGA MWINGI MAONESHO YA SABASABA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here