Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.
KIUNGO wa timu ya Taifa Zambia Rainford Kalaba atakuwa sehem ya wachezaji 23 wa TP Mazembe wanaotarajia kuja September 18 Kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Simba Katika tamasha la Simba day litakalofanyika Jumapili Katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo nyota huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji wakongwe wa timu hiyo atakuwa sehemu ya msafara huo ambao pia utakuwa na viongozi 12 na kufanya msafara huo kuwa na watu 35.
Pia Simba imekuwa na mahusiano mazuri na timu hiyo kutoka Congo na mara kadhaa imekuja ikicheza nayo michezo ya kirafiki,lakini pia mara ya mwishon kikosi hicho kuja nchini ni mwanzoni mwa mwaka huu ambapo ilikuja kishiriki mashindano ya Super Cup yaliyoandaliwa na Simba.