Home LOCAL DC MSANDO WAMACHINGA WATAPA MAENEO BILA RUSHWA LEO

DC MSANDO WAMACHINGA WATAPA MAENEO BILA RUSHWA LEO

NA: HERI SHAABAN

MKUU wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema Wafanyabiashara Wamachinga wa Manispaa ya Morogoro watagaiwa maeneo yao ya biashara bila kutoa rushwa.

Mkuu wa Wilaya Albert Msando alitoa taarifa hiyo leo katika mitandao  ya kijamii akieleza kutekeleza agizo la Serikali kuwatengea maeneo ya Biashara Wamachinga wa Manispaa ya Morogoro.

“Katika Wilaya yangu natekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Hassan Suluhu, tutawagawia wafanyabiashara wetu maeneo kwa kufuata taratibu bila fujo ” alisema Msando.

Mkuu wa Wilaya Msando alisema wafanyabiashara wa Manispaa hiyo wa 

Isalam, Mlapakolo ,Madaraka,Uhuru,na Luna  watamia eneo la Soko Kuu Chifu Kingalu.

Taarifa hiyo ilisema wafanyabiashara watakaogaiwa eneo la biashara ni wamachinga walioandikwa majina na viongozi wao wa mitaa na walihakiki wenyewe majina yao kwa utaratibu huliowekwa . 

Utaratibu wa kugawa maeneo ni wa WAZI. Mabanda yote yana namba,Ugawaji ni kutumia mfumo wa bahati nasibu. Utaokota namba kwenye pipa/box utaenda ilipo namba uliyookota. 

Taarifa hiyo ilisema kuwa hakuna  upendeleo zoezi hilo  litasimamiwa na mkuu wa Wilaya mwenyewe hivyo wananchi wafanyabiashara wawe makini wasitapeliwe wala kutoa rushwa wote wana haki sawa .

HAKUNA yeyote atakayepewa nafasi kama hakuandikwa jina kwenye mtaa aliopo sasa na kila MTU atakikiwa jina lake . 

Aidha Taarifa hiyo ilisema kuwa hakuna mfanyabiashara  atakayepewa banda au meza ili amkodishie mtu mwingine na kumnyonya kodi pia alisema maeneo yasitengwa kwa biashara airusiwi kufanya biashara

Mwisho

Previous articleKALABA KUIONGOZA TP MAZEMBE SIMBA DAY
Next articleKEVELA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KULETA UWIANO WA KIJINSIA KATIKA UTEUZI WA VIONGOZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here