Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (wa tatu kulia) akiwa na Rais wa Taasisi hiyo Stigimana Tenga (katikati) na mwenyekiti wa Bodi ya FCS DKT Richard Samabiga (wa kwanza kulia) wakiangalia mpango mkakati utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano mara baada ya kufanyika uzinduzi rasmi wa mpango huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ofisi za FCS Jijini Dar es Salaam.
Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kushikamana kwa pamoja na kuhakikisha wanazisemea kazi wanazofanya katika Taasisi zao ili ziweze kufahamika kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
Pia amezitaka Asasi hizo kuhakikisha wanaangalia mifumo mbalimbali inayowaongoza ambayo ndio miundombinu ya uwajibikaji katika kazi zao hususani katika kutatua matatizo ya wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati mpya wa Foundation For Civil Society (FCS) RAIS wa Taasisi hiyo Dkt. Stigmata Tenga amesema kuwa Asasi za Kiraia zinapaswa kujengwa kutokana kuwa ni muhimili mkubwa wa maendeleo nchini nakwamba wananchi wanapaswa kuzifahamu.
Aliongeza kuwa Asasi zinapaswa kutatua matatizo ya wananchi na kusaidia kuyaondoa hilo ndio lengo kubwa la FCS katika Dira yake.
“Tujenge uwajibikaji katika misingi ya ubinadamu na utu bila kujali kuna nini, bali kuwashirikisha wenzetu matatizo ambayo sekta ya Asasi za kiraia nchini inapitia ambayo yanahitaji kutatuliwa kwani ni matatizo yanayojikita katika mifumo,” Aliongeza Dkt. Tenga
Aidha alisema hawapaswi kutatua matatizo kwa mbinu zile zile za zamani ambazo sio mbinu za kujenga mifumo bali ni mbinu za kutoa huduma.
“Tusipoangalia hivyo tutazidi kuona hizo mbinu zinaongezeka na kuwa kubwa sana na kuhakikisha wanaangalia mifumo ambayo ndio miundombiniu ya uwajibikaji katika Aaasisi,” alisema
Kwa Upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga alisema kuwa wamezindua mpango mkakati mpya wa FCS ambao unalenga kushuka chini hususani vijijini katika kuwasaidia wananchi.
Alisema farsafa ya Taasisi yao inaamini kuwa umasikini,hali ya kutokuwa na haki katika jamii,hali ya ukandamizaji watu wengine ni tatizo kubwa na ni adui wakubwa wa maendeleo.
Alisema katika rasilimali zao takribani asilimia 90 inakwenda vijijini kuhudumia wananchi “Rasilimari zetu tunavyogawa kila mwaka asilimia 90 inakwenda vijijini tunaamini waliopo Dar es Salaam ,Taasisi nyingi zinaweza kufanya kazi na watu wengine kokote duniani,kuliko waliopo vijijini” alisema Kiwanga
Pia aliongeza kwa kusema kuwa katika mpangokazi wao wanazingatia usawa wa kijinsia,kufanya kazi na wadau wao kuwapa heshima inayostahili na kuwaheshimu kwani wao ndio wabia wao wakubwa na kwamba sauti yao ina ukubwa wa kuweza kuwafikia wananchi.
Baadhi ya watumishi WA FCS na wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye hafla ya Uzi duzi huo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi za kiraia, Dkt.Richard Samabiga aliipongeza FCS kwa hatua hiyo ya kuzindua mpango mkakati huo ambao unaonyesha dira ya kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali.
Alisema mpango huo unaleta matumaini makubwa kwa Asasi za kiraia katika kufanya kazi zao za kusaidia wananchi.
Mpango mkakati huo umejikatika katika kutekeleza miradi ya utawala bora, usawa wa kijinsia na watu wenye ulemavu, kukuza uchumi na kujenga amani na utatuzi wa migogoro.