Home LOCAL FCS YAZINDUA MPANGO MKAKATI MPYA WA MIAKA MITANO

FCS YAZINDUA MPANGO MKAKATI MPYA WA MIAKA MITANO

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (wa tatu kulia) akiwa na Rais wa Taasisi hiyo Stigimana Tenga (katikati) na mwenyekiti wa Bodi ya FCS DKT Richard Samabiga (wa kwanza kulia) wakiangalia mpango mkakati utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano mara baada ya kufanyika uzinduzi rasmi wa mpango huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ofisi za FCS Jijini Dar es Salaam.


Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kushikamana kwa pamoja na kuhakikisha wanazisemea kazi wanazofanya katika Taasisi zao ili ziweze kufahamika kwa wananchi na jamii kwa ujumla.

Pia amezitaka Asasi hizo kuhakikisha wanaangalia mifumo mbalimbali inayowaongoza ambayo ndio miundombinu ya uwajibikaji katika kazi zao hususani katika kutatua matatizo ya wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati mpya wa Foundation For Civil Society (FCS) RAIS wa Taasisi hiyo Dkt. Stigmata Tenga amesema kuwa Asasi za Kiraia zinapaswa kujengwa kutokana kuwa ni muhimili mkubwa wa maendeleo nchini nakwamba wananchi wanapaswa kuzifahamu.

Rais. wa FCS Dkt. Stigimana Tenga akizungumia mpango huo mara baada ya kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

“Tuisemee sekta hii na yale yote ambayo sekta hii inayafanya kwenye jamii, yasemeeni mnayoyafanya ili yajulikane msione aibu yeyote,”alisema Dkt. Tenga.

Aliongeza kuwa Asasi zinapaswa kutatua matatizo ya wananchi na kusaidia kuyaondoa hilo ndio lengo kubwa la FCS katika Dira yake.

“Tujenge uwajibikaji katika misingi ya ubinadamu na utu bila kujali kuna nini, bali kuwashirikisha  wenzetu matatizo ambayo sekta ya Asasi za kiraia nchini inapitia  ambayo yanahitaji kutatuliwa kwani ni matatizo yanayojikita katika mifumo,” Aliongeza Dkt. Tenga 

Aidha alisema hawapaswi kutatua  matatizo kwa mbinu zile zile za zamani ambazo sio mbinu za kujenga mifumo bali ni mbinu za kutoa huduma.

“Tusipoangalia hivyo tutazidi kuona hizo mbinu zinaongezeka na kuwa kubwa sana  na kuhakikisha wanaangalia mifumo ambayo ndio miundombiniu ya uwajibikaji katika Aaasisi,” alisema

Kwa Upande wake,Mkurugenzi Mtendaji  wa FCS Francis Kiwanga alisema kuwa wamezindua mpango mkakati mpya wa FCS ambao unalenga kushuka chini hususani vijijini katika kuwasaidia wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo akielezea namna ambavyo FCS itavyotekeleza majukumu yake Katika kuusimamia mpango huo.


Alisema kupitia mpango huo Taasisi yao itaendelea kufanya kazi na Asasi mbalimbali za kiraia ambao ndio wadau wao muhimu katika kuwafikia wananchi.

Alisema farsafa ya Taasisi yao inaamini kuwa umasikini,hali ya kutokuwa na haki katika jamii,hali ya ukandamizaji watu wengine ni tatizo kubwa na ni adui wakubwa wa maendeleo.

Alisema katika rasilimali zao takribani asilimia 90 inakwenda vijijini kuhudumia wananchi “Rasilimari zetu tunavyogawa kila mwaka asilimia 90 inakwenda vijijini tunaamini waliopo Dar es Salaam ,Taasisi  nyingi zinaweza kufanya kazi na watu wengine kokote duniani,kuliko waliopo vijijini” alisema Kiwanga

Pia aliongeza kwa kusema kuwa katika mpangokazi wao wanazingatia usawa wa kijinsia,kufanya kazi na wadau wao kuwapa heshima inayostahili  na kuwaheshimu kwani wao ndio wabia wao wakubwa na kwamba sauti yao ina ukubwa wa kuweza kuwafikia wananchi.

Baadhi ya watumishi WA FCS na wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye hafla ya Uzi duzi huo.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi za kiraia, Dkt.Richard Samabiga aliipongeza FCS kwa hatua hiyo ya kuzindua mpango mkakati huo ambao unaonyesha dira ya kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali.

Alisema mpango huo unaleta matumaini makubwa kwa Asasi za kiraia katika kufanya kazi zao za kusaidia wananchi.

Mpango mkakati huo umejikatika katika kutekeleza miradi ya utawala bora,  usawa wa kijinsia na watu wenye ulemavu, kukuza uchumi na kujenga amani na utatuzi wa migogoro.  

Previous articleBENKI YA ABSA TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO KWA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA AT TAAUN
Next articleZAKA: AZAM IPO IMARA DHIDI YA POLISI TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here