Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inawapongeza wanariadha wetu Kpt. Magdalena Shauri na Sgt. Alphonce Simbu kwa kushinda mbio za Mashindano ya Majeshi Abuja nchini Nigeria.
Wanariadha wote wawili wameshinda Mbio za full Marathon za Kilomita 42.19, ambapo Alphonce Simbu amekimbia kwa muda wa saa 2, dakika 17 na sekunde 19 (2:17:19) wakati Magdalena Shauri ameshinda kwa muda wa saa 2, dakika 36 na sekunde 29 (2:36:29) na wote wamepata medali za dhahabu.
http://HONGERENI WANARIADHA WA TANZANIA KWA KUSHINDA MEDALI ZA DHAHABU