Home SPORTS ZAKA: AZAM IPO IMARA DHIDI YA POLISI TANZANIA

ZAKA: AZAM IPO IMARA DHIDI YA POLISI TANZANIA

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

UONGOZI wa  Azam Fc  umesema kuwa unaendelea na mazoezi ili kufanya  vyema katika mchezo wao dhidi ya polisi Tanzania utakaopigwa katika dimba la Karatu.

Kauli hiyo ilitolewa  na Ofisa habari wa kikosi hicho Zaka zakazi alisema kuwa wachezaji wapo vizuri na wana morali ya kutosha katika kuhakikisha wanajinyakulia pointi tatu muhimu.

“Kikosi kipo tayari moshi kwa ajili ya mchezo huo lakini pia mchezaji poul katema alipata majeraha katika mchezo wetu dhidi ya Coastal united lakini amejiunga na mazoezi,kikosi chote kipo salama na sasa tunajipanga vyema”

Aliongeza kuwa jambo la kutoka sare  dhidi ya Coastal Union  hayakuwa mabaya  kwani mchezo ulikuwa wa haki japo sasa tunajipanga kucheza vyema na kupata ushindi.

Licha ya kwamba Polisi hawajawahi tuifunga Azam hivyo tunazidi kujihimarisha ili kupata matokeo katika mchezo huo

Previous articleFCS YAZINDUA MPANGO MKAKATI MPYA WA MIAKA MITANO
Next articleKAMPUNI YA ULINZI YA SGA YAPATA TUZO YA JUU KATIKA MAONESHO YA MADINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here