Home BUSINESS NARCO WAWEZESHENI WANANCHI KUFUGA KIBIASHARA – CHONGOLO

NARCO WAWEZESHENI WANANCHI KUFUGA KIBIASHARA – CHONGOLO

Kampuni ya Rachi za Taifa – NARCO imetakiwa kuwawezesha zaidi wafugaji wadogo ili watoke katika kilimo cha kawaida na wafikie daraja la kilimo cha Biashara.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alipotembelea NARCO Ranchi ya Kongwa,Mkaoni Dodoma katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Akizungumza katika Ranchi hiyo Chongolo amesema kuna wafugaji ambao wana mifugo mingi lakini haiwafaidishi kutokana na kukosa elimu ya Ufugaji kibiashara, na kutumia mazao ya Ng’ombe kama ngozi na Pembe katika matumizi yasiyo na tija kwao.

Aidha ameagiza kupelekwa mbegu maeneo ya malisho ya wakulima wa kawaida ili kulima mazao ya Ng’ombe yatakayosaidia katika malisho,hasa katika kipindi cha kiangazi ambacho kuna changamoto ya malisho.

Kwa upende wake Mkurugenzi wa NARCO Peter Msofe ameiomba Serikali kuwawezesha katika Miradi miwili yenye thamani ya Bilioni 84 yenye lengo la kutoa Elimu kwa Wanawake na Vijana kuhusu ufugaji pamoja na mradi wa unenepeshaji ng’ombe.

Ranchi hiyo ya Kongwa ina Hekta 38,000 ambapo ndani yake kuna Mifugo 30000,huku Hekta 18,000 wakipewa wawekezaji wakiwemo wananchi.

Previous articleCHONGOLO ATAKA MRADI WA VIJANA WA KILIMO KUKAMILIKA AGOSTI MWAKA HUU
Next articleTANTRADE, TANROADS WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA VIWANJA VYA MAONESHO YA SABASABA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here