Home BUSINESS TANTRADE, TANROADS WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA VIWANJA VYA MAONESHO YA SABASABA.

TANTRADE, TANROADS WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA VIWANJA VYA MAONESHO YA SABASABA.

15 Juni, 2023,  Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Wakala wa Barabara Tanzania (TanRoads) kuboresha na kukarabati miundo mbinu ya ndani na nje ya Uwanja wa Maonesho wa mwl. J.K Nyerere uliopo barabara ya Kilwa Dar es salaam.

Kikao kazi hicho kimefanyika 15 Juni, 2023, katika ofisi za TanTrade Dar es salaam na kuhudhuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania bi. Latifa M. Khamis, na Wataalam kutoka Tanroads Mhandisi Haruin Rashid Senkuku, Mhandisi Elisony Edward Mweladzi, Mhandisi Raymond Godfrey Maimu pamoja na wajumbe wa mkutano huo kutoka TanTrade.

Akiongea katika kikao hicho, bi. Latifa amesema tumeamua kushirikiana na Tanroads katika kuboresha miundo mbinu ya Uwanja ili kuchochea mabadiliko makubwa na kuyapa zaidi mvuto maonesho ya mwaka huu pamoja na kuleta urahisi wa kufanya biashara.

“Lengo ni kuendelea kuboresha miundombinu ya Maonesho ili kuweka Mazingira mazuri ya uoneshaji wa bidhaa kwa Wafanyabiashara pamoja na Watembeleaji na kuleta matokeo yenye tija” alisema.

Previous articleNARCO WAWEZESHENI WANANCHI KUFUGA KIBIASHARA – CHONGOLO
Next articleRAIS DK.MWINYI AHUDHURIA UFUNGUZI WA OLIMPIKI MAALUM BERLIN
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here