Timu za Argentina na Ufaransa zimetoshana nguvu katika dakika 90 za Mchezo wa Fainali wa Kombe la Dunia unaopigwa nchini Qatar.
Timu ya Argentina ndio walikuwa wa kwanza kuzichana nyavu za Ufaransa kwa mabao mawili yaliyofungwa na Lionel Messi na Angelo Di Maria.
Kipindi cha pili Kilian Mbape alipachika mabao yote mawili likitanguliwa na bao la mkwaju wa Penati na dakika chache baadae kutupia bao la kusawazisha na kilazimika kwenda hatua ya dakika 30 za kuongeza.